Hospital
Hospital ya Muhimbili Yafanikisha UPASUAJI wa kwanza wa kutenganisha MAPACHA
Hospital ya Muhimbili Yafanikisha
UPASUAJI wa kwanza wa kutenganisha
MAPACHA walioungana AINA YA PARASITIC CONJOINED TWINS.
Madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agosti 6, 2026, wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza wa kutenganisha mapacha
walioungana aina ya parasitic conjoined twins, ambapo mmoja wa mapacha hakukua kikamilifu na alikuwa akimtegemea mwenzake kwa ukuaji na uhai wake.
Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Dkt. Victor Ngotta, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa MNH, amesema mafanikio hayo yanaonyesha
uwezo wa hospitali kushughulikia kesi ngumu na adimu zinazohitaji utaalamu wa hali ya juu, na ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha huduma
za upasuaji wa kibingwa nchini.
Dkt. Ngotta amesema upasuaji huo ulihitaji maandalizi ya kina na ushirikiano wa wataalamu kutoka fani mbalimbali kutokana na hali ya kipekee
ya mtoto huyo, ambaye alikuwa na pacha aliyekuwa na mikono, miguu na sehemu ya kiuno pekee huku akimtegemea mwili wa mwenzake kwa ukuaji na Mafanikio ya upasuaji huo yanaendelea kuimarisha nafasi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kama kituo
kinachoongoza nchini katika utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.
Credits: https://www.instagram.com/p/Db2yJZDjdAU/img_index=1&igsh=MndnOGZ3aGhyajlw
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa