Connect with us

Uzazi/Ujauzito

Kifafa cha Mimba:Chanzo, Dalili, Tiba na Hatari kwa Mama na Mtoto

Doctor Ombeni

Published

on

281 Views
0 Comments

Tatizo la Kifafa cha mimba, kitaalamu hujulikana kama eclampsia, ni hali hatari inayoweza kumpata mwanamke wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au hata baada ya kujifungua. Hali hii hutokea pale mwanamke anapowa na tatizo la shinikizo la juu la damu linalohusiana na ujauzito,pamoja na uwepo wa Proteins kwenye Mkojo, Dalili zake ni pamoja na Mtu kupata hali ya kutingishika au kutetemeka(fitts)degedege(seizures) pamoja na dalili zingine kama kuvimba sana uso,miguu,mikono n.k.

Kwahiyo Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba pre-eclampsia/Eclampsia huhusisha mambo makuu mawili(Criteria):

  1. Shinikizo la juu la Damu: Diastolic blood pressure(BP) 110mm Hg au Zaidi
  2. Uwepo wa Proteins kwenye Mkojo: Proteinuria 2+ au Zaidi

Chanzo cha Kifafa cha Mimba

Chanzo halisi cha pre-eclampsia na eclampsia hakijulikani kikamilifu. Hata hivyo kwa baadhi ya tafiti, tatizo hili linahusishwa na namna kondo la nyuma la mtoto (placenta) linavyoundwa na kuingiliana na mishipa ya damu ya mama. Mabadiliko hayo yanaweza kusababisha mishipa ya damu kubana, shinikizo la damu kupanda na viungo mbalimbali vya mwili kuanza kuathirika.

Mwanamke anaweza kuwa katika hatari zaidi ikiwa:

  • ni mimba yake ya kwanza,
  • ana ujauzito wa watoto wawili au zaidi,
  • ana historia ya pre-eclampsia katika ujauzito uliopita,
  • ana shinikizo la damu, kisukari au ugonjwa wa figo,
  • ana uzito mkubwa kupita kiasi,
  • au ana historia ya kuwa kwenye familia yenye tatizo hili la pre-eclampsia.

Dalili Kuu za Kifafa cha Mimba

Kabla ya kifafa kutokea, mwanamke anaweza kuwa na dalili za pre-eclampsia. Dalili zinazopaswa kuchukuliwa kwa uzito ni pamoja na:

1.Kupata Maumivu makali ya kichwa yasiyopungua, maumivu haya makali ya Kichwa hutokea hasa hasa kwa Mbele au pembeni

2.kuona ukungu au Marue rue,”Blurr vission”

3.Kupata maumivu makali sehemu ya juu ya tumbo hasa upande wa kulia,

4.kuvimba sana miguu, uso na mikono,

5.Kupata kichefuchefu au kutapika baada ya kipindi cha mwanzo cha ujauzito,

6. Pamoja na Ishara hizi kuu- shinikizo la damu kuwa juu na Uwepo wa Proteins kwenye Mkojo.

Fahamu,Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na shinikizo la damu la juu au pre-eclampsia bila kuwa na dalili zinazoonekana, ndiyo maana vipimo vya kliniki kwa wajawazito ni muhimu.

Kifafa cha mimba ni dharura ya kitabibu. Mwanamke anayepata degedege akiwa mjamzito au muda mfupi baada ya kujifungua anapaswa kupelekwa hospitalini haraka, hata kama degedege imeacha yenyewe.

Takwimu za Tanzania Zinaonyesha Tatizo Hili Ni Muhimu kulizingatia:

Takwimu za Wizara ya Afya Tanzania zinaonyesha uzito wa Tatizo la Kifafa cha Mimba(pre-eclampsia na eclampsia) katika vifo vya kina mama nchini. Katika uchambuzi wa vifo vya kina mama vilivyorekodiwa katika kipindi cha 2018–2023, pre-eclampsia/eclampsia zilihusishwa na takribani 14.1% ya vifo vya kina mama vilivyoainishwa kwenye sababu za ICD-10. Hii iliifanya kuwa miongoni mwa sababu kubwa za vifo vya kina mama nchini, baada ya tatizo la kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.

Katika kipindi hicho, Wizara ya Afya ilirekodi jumla ya vifo 9,668 vya kina mama, huku 93% ya vifo hivyo, sawa na 8,998, vikitokea katika vituo vya kutolea huduma za afya. Pia, institutional maternal mortality ratio ilishuka kutoka 94 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2018 hadi 65 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2023.

Utafiti uliochambua takwimu za mfumo wa DHIS-2 Tanzania kwa mwaka 2016–2020 pia ulionyesha kuwa eclampsia iliripotiwa miongoni mwa matatizo ya ujauzito katika vituo vya afya. Kiwango kilichoripotiwa kilikuwa takribani 0.3% mwaka 2016 na 2017, na 0.2% mwaka 2018 hadi 2020.

Kwa dunia nzima, WHO inakadiria kuwa pre-eclampsia huathiri takribani 3–8% ya wanawake wanaojifungua, na matatizo ya shinikizo la damu wakati wa ujauzito yanahusishwa na takribani 16% ya vifo vyote vya kina mama duniani. Mwaka 2023, hii ililingana na takribani vifo 42,000.

Kifafa cha Mimba Kinavyotibiwa

Tatizo la Kifafa cha Mimba au Eclampsia halitibiwi nyumbani. Mwanamke anahitaji huduma ya haraka hospitalini kwa sababu lengo la kwanza ni kuzuia degedege kurudia, kudhibiti shinikizo la damu, kulinda viungo vya mama na kumsaidia mtoto, huku timu ya afya ikitathmini muda na namna salama ya kujifungua.

Dawa muhimu inayotumika kuzuia na kutibu degedege inayohusiana na tatizo hili la Kifafa cha Mimba au eclampsia ni magnesium sulfate. WHO inaeleza kuwa magnesium sulfate inaweza kupunguza hatari ya pre-eclampsia kuendelea kuwa eclampsia kwa zaidi ya nusu.

Madaktari pia hutumia dawa za kushusha shinikizo la damu pale shinikizo linapokuwa juu kwa kiwango hatari. Mama hufuatiliwa kwa karibu, ikiwa ni pamoja na hali ya shinikizo la damu, hali ya figo na ini, mkojo, vipimo vya damu na hali ya mtoto tumboni.

Uamuzi wa kujifungua hutegemea hali ya mama, umri wa mimba, hali ya mtoto na ukali wa ugonjwa. Katika baadhi ya wanawake, ujauzito unaweza kufuatiliwa kwa karibu ikiwa hali imetulia na mtoto bado hajawa tayari kuzaliwa; lakini ikiwa mama ana eclampsia au pre-eclampsia kali isiyodhibitika, timu ya madaktari inaweza kuamua kuharakisha kujifungua baada ya kumtuliza mama.

WHO pia inapendekeza matumizi ya corticosteroids katika mazingira ambayo kujifungua kabla ya wakati kunatarajiwa, ili kusaidia ukomavu wa mapafu ya mtoto.

Hospitali Tanzania Zinazoweza Kutoa Huduma

Huduma za usimamizi wa mimba kwa Wajawazito wenye shinikizo la juu la damu, ikiwemo kwa matatizo kama vile Kifafa cha Mimba/pre-eclampsia/eclampsia), zipo katika mfumo wa huduma za afya Tanzania. Mfumo rasmi wa Tanzania Health Facility Registry wa Wizara ya Afya unaonyesha vituo mbalimbali vilivyosajiliwa kutoa huduma za usimamizi wa mimba zenye shinikizo la damu/pre-eclampsia.

Kwa Mwanamke mwenye hali kali au dalili za dharura anaweza kutafuta huduma katika hospitali Zote zenye huduma za uzazi.

Hata hivyo, katika tukio la degedege, si muhimu kusubiri kwenda hospitali fulani. Kitu muhimu ni kumfikisha mama katika kituo cha afya chenye uwezo wa kushughulikia dharura ya uzazi haraka iwezekanavyo.

Je, Kifafa cha Mimba Kinaweza Kuzuiwa?

Hatari inaweza kupunguzwa kwa kuanza kliniki ya ujauzito mapema na kuhudhuria mahudhurio yote yailliyopangwa. Katika kliniki, shinikizo la damu hupimwa na mkojo unaweza kupimwa kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa uwepo wa protini kwenye Mkojo(proteinuria). Uchunguzi wa mara kwa mara unaweza kusaidia kugundua pre-eclampsia kabla haijawa eclampsia.

Kwa wanawake walio katika hatari kubwa, daktari anaweza kupendekeza aspirin ya dozi ndogo wakati wa ujauzito, kulingana na tathmini ya hatari. WHO pia inapendekeza kuzingatia calcium supplementation kwa wajawazito katika maeneo yenye ulaji mdogo wa calcium. Hizi hazipaswi kuanza bila ushauri wa mtoa huduma wa afya.

Muhimu zaidi, mwanamke mjamzito hapaswi kupuuza maumivu makali ya kichwa, kuona ukungu au Marue rue, maumivu makali juu ya tumbo, shinikizo la damu kuwa juu, degedege au kupoteza fahamu. Dalili hizi zinaweza kuashiria hali inayohatarisha maisha ya mama na mtoto.

Kumbuka: Kifafa cha mimba si kifafa cha kawaida cha muda mrefu. Ni dharura inayohusishwa na ujauzito na shinikizo la damu, na inahitaji matibabu ya hospitali. Mwanamke anayepata degedege wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua anapaswa kupata huduma ya dharura mara moja.

References:

281 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume:...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist)  PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania,...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya...

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, FACTS checked by Dr.Joseph(gynecologist) Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO)...

282
0