Connect with us

Afya News

Mwitikio Dhidi Ya Tahadhari Kujikinga na Ugonjwa Wa Ebola waendelea kuimarishwa nchini

Avatar

Published

on

130 Views
0 Comments

Mwitikio Dhidi Ya Tahadhari Kujikinga na Ugonjwa Wa Ebola waendelea kuimarishwa nchini

Na Cletus Sanga, WAF – Arusha

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya waziri Mkuu – TAMISEMI na CIHEB Tanzania chini ya Mradi wa Usalama wa Afya Duniani unaofadhiliwa na serikali ya Marekani imeendelea kuimarisha mwitikio dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa kuendesha zoezi la kuigiza hali halisi ya mlipuko, likilenga kupima uwezo wa wataalamu wa afya na mifumo ya uratibu katika kutoa mwitikio wa haraka, salama na wenye ufanisi endapo kutatokea tishio la ugonjwa huo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo tarehe 08 Agosti, 2026, Mratibu wa zoezi na Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya, Bi. Theresia Haule, amesema mazoezi ya aina hiyo ni muhimu katika kupima uwezo wa wataalamu wa afya kutumia maarifa na ujuzi walioupata katika mazingira yanayofanana na hali halisi ya mlipuko wa Ebola.

Bi. Haule amesema zoezi hilo linasaidia kubaini maeneo yenye mafanikio na yale yanayohitaji kuimarishwa ili kuhakikisha mifumo ya utoaji huduma inakuwa tayari kutoa mwitikio wa haraka na wenye ufanisi wakati wowote panapotokea dharura ya afya ya umma.

Ameongeza kuwa kupitia zoezi hilo, wataalamu wa afya wameendelea kuimarisha uelewa wa taratibu za kukabiliana na Ebola, ikiwemo utambuzi wa wagonjwa wenye dalili za ugonjwa huo, utoaji wa taarifa kwa wakati, udhibiti wa maambukizi, matumizi sahihi ya vifaa kinga binafsi pamoja na uratibu wa huduma kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mradi wa Usalama wa Afya Duniani kutoka CIHEB Tanzania, Dkt. Edgar Lusayo, amesema mazoezi ya kuigiza hali halisi ya mlipuko wa Ebola ni sehemu muhimu ya kuendelea kujenga uwezo wa wataalamu wa afya na kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na wadau wa maendeleo katika kujiandaa kukabiliana na dharura za afya ya umma.

Dkt. Lusayo ameongeza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha mifumo ya utayari na mwitikio wa magonjwa ya mlipuko kwa kutoa msaada wa kiufundi, mafunzo na uwezeshaji wa mazoezi ya vitendo, hatua itakayochangia kulinda afya za wananchi na kuimarisha usalama wa afya nchini.

This post @reshared from @wizara_afyatz.

130 Views
0 Comments
✚

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital warts ni moja ya aina...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu Tatizo la...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

 PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake) PID NI NINI?  PID...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya kidonda mara moja. Mchakato huu...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa wa kuambukiza sana kwa watoto...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi mkubwa baada ya watoto wawili...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali kupitia chama chao cha wafanyakazi....

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya tumbaku yana athari kubwa kwa...

131
0