Connect with us

magonjwa yasioyakuambukiza

Tatizo la Overactive Bladder,Dalili na Sababu zake

afyaclass

Published

on

🩺

Overactive Bladder – (OAB) ni hali ya kiafya inayomfanya mtu ahisi hamu ya kukojoa ghafla na kwa nguvu, kiasi kwamba ni vigumu Mtu kuizuia mkojo. Hali hii inaweza kuathiri watu wa rika mbalimbali na huweza kuvuruga shughuli za kila siku pamoja na Usingizi wakati wa usiku.

Kwa mujibu wa taarifa za Mayo Clinic, dalili kuu ya Overactive Bladder – (OAB) ni hamu ya kukojoa inayotokea ghafla na ambayo ni vigumu kuidhibiti. Wakati mwingine hali hii inaweza kusababisha mkojo kutoka bila kukusudia kabla mtu hajafika chooni.

Dalili za Tatizo la Overactive Bladder

Dalili zinazoweza kuashiria Overactive Bladder – (OAB) ni pamoja na:

  • Kuhisi hamu ya kukojoa ghafla na kwa nguvu ambayo ni vigumu kuizuia.
  • Mkojo kutoka bila kujizuia baada ya kupata hamu kali ya kukojoa (urge incontinence).
  • Kukojoa mara nyingi, yaani mara nane au zaidi ndani ya saa 24.
  • Kuamka usiku zaidi ya mara mbili kwenda kukojoa (nocturia).

Dalili hizi zinaweza kuathiri uwezo wa kufanya kazi, kusafiri, kushiriki shughuli za kijamii na hata kupata usingizi wa kutosha.

Ni lini unapaswa kumuona daktari?

Ni muhimu kutafuta ushauri wa daktari ikiwa:

  • Unakojoa mara nyingi kuliko kawaida bila sababu inayoeleweka.
  • Hamu ya kukojoa inakuzuia kufanya shughuli zako za kila siku.
  • Unashindwa kuzuia mkojo mara kwa mara.
  • Unaamka mara nyingi usiku kwa ajili ya kukojoa.

Daktari anaweza kupendekeza vipimo ili kubaini chanzo cha tatizo na kupendekeza matibabu au mbinu za kulidhibiti.

Facts:

Ingawa tatizo la Overactive Bladder – (OAB) si ugonjwa unaotishia maisha moja kwa moja, Tatizo hili Linaweza kuleta Usumbufu kwenye maisha ya Mtu ikiwa halitatambuliwa na kutibiwa Mapema. Kutambua dalili mapema na kupata ushauri wa kitaalamu kunaweza kusaidia kudhibiti hali hii na kuboresha maisha ya mgonjwa.

Reference:

  • Mayo Clinic. Overactive bladder – Symptoms and causes.

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Ushauri & Tiba,Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *