Connect with us

Hospital

Ugonjwa wa Homa ya Ini unaoweza kukaa mwilini kwa miaka bila dalili

Avatar

Published

on

Photo Credits:Dkt. Swaleh Kitabu Pazi, Daktari Mbobezi wa magonjwa ya Mfumo Chakula na Ini kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, nchini Tanzania.
148 Views
0 Comments

Ugonjwa wa Homa ya Ini unaoweza kukaa mwilini kwa miaka bila dalili

Virusi vya Homa ya Ini vinaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu bila kuonesha dalili, huku vikiendelea kuliharibu ini na kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani.

Onyo hilo lilitolewa na Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, nchini Tanzania Dkt. Swalehe Kitabu Pazi, katika siku ya maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani tarehe 28 Julai inayolenga kutoa elimu kwa umma kuhusu ugonjwa huo.

Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Dkt. Pazi amesema homa ya ini husababishwa na virusi vya aina mbalimbali, lakini virusi vya homa ya ini B na C ni miongoni mwa vinavyoweza kusababisha madhara makubwa visipotibiwa.

“Unaweza ukahisi kwamba uko salama, lakini ugonjwa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika mwili,” amesema.

Ameeleza kuwa kugundua ugonjwa mapema humwezesha mgonjwa kuanza kufuatiliwa na kupata matibabu kabla ini halijapata madhara makubwa.

Saratani ya ini inapogunduliwa katika hatua za mwanzo inaweza kutibiwa, lakini mgonjwa akichelewa kufika hospitalini huenda akabaki na tiba za kupunguza makali ya ugonjwa na kurefusha maisha pekee.

Jinsi ya kulinda afya ya ini
Dkt. Pazi amewataka wananchi kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa ya ini kwa kufanya ngono salama na kuepuka matumizi ya vifaa vinavyoweza kuwa na damu ya mtu mwingine.

Pia amesisitiza umuhimu wa wanawake wajawazito kupima, kwa kuwa virusi vya homa ya ini B vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.

Kupunguza au kuacha matumizi ya pombe na sigara pia kunaweza kusaidia kulinda ini dhidi ya madhara.

Fahamu Pia,Chanjo inapatikana kwa ajili ya kuzuia homa ya ini B, huku homa ya ini C ikiwa na dawa zinazoweza kuitibu.

Wananchi wahimizwa kwenda kupima,Wananchi wamehimizwa kupima na kufahamu afya ya ini, hata kama hawana dalili zozote.

“Kupima kunasaidia kugundua tatizo katika hatua za mwanzo. Ukijua afya yako, inakuwa rahisi kupata matibabu yanayofaa,” amesema Dkt. Pazi.

#Soma Ugonjwa wa Homa ya Ini Pamoja na Dalili Zake Hapa

References:

148 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. Ugonjwa...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. VIPELE...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi.  PID...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. DALILI...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. Mamlaka...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. UGONJWA...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. Ugonjwa...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. Mlipuko...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. Wauguzi...

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Content Via Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula,Dkt. Swalehe Kitabu Pazi. Uvutaji...

149
0