Connect with us

Afya News

Wanawake kutozwa Sh. 500, kwa ajili ya kununua mzani wa watoto kliniki

Avatar

Published

on

Image with: Marco Maduhu
111 Views
0 Comments

Wanawake kutozwa Sh. 500, kwa ajili ya kununua mzani wa watoto kliniki.

WANAWAKE wa Kijiji cha Nyashimbi, Kata ya Puni, wilayani Shinyanga, wamelalamikia kutozwa Sh. 500, kwa ajili ya kununua mzani wa kupimia uzito watoto wanapowapeleka kliniki.

Malalamiko hayo yametolea jana, katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, uliofanyika kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majibu.

Mmoja wa wanawake hao, Eva Mbeshi, mkazi wa Kitongoji cha Kigwang’hona, Kijiji cha Nyashimbi, amesema wamekuwa wakihangaika kupata huduma ya kliniki ya kupima uzito wa watoto, kutokana na mzani kuharibika na kuambiwa wachange Sh. 500 kwa ajili ya kununua mwingine mpya.

“Tuna miezi miwili watoto wetu hawajapimwa uzito hadi tutoe hiyo Sh. 500, ili kununua mzani mwingine mpya,” amesema Eva.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Nyashimbi, Stephano Masinga, amekiri mzani wa kupimia uzito watoto kuwa umeharibika na kwamba alishaandika ombi la kupata mzani mwingine kutoka Bohari ya Dawa (MSD), lakini licha ya kuagiza zaidi ya mara tatu mzani huo hawajaupata.

Amesema, baada ya kuona hawapati mzani huo, kutoka bohari ya dawa, ndipo wakaona ili kuendelea kutoa huduma hiyo, ni vyema wananchi wakachangia sh. 500 ili wanunue mzani mpya na watoto waendelee kupimwa uzito.

Mbunge wa Jimbo hilo la Itwangi, Azza, amesema yeye kama mwakilishi wa wananchi, atanunua mzani huo kwa fedha zake mwenyewe na kuukabidhi ndani ya wiki moja, ili watoto waendelee kupata huduma za kliniki na kupimwa uzito.

“Nimekaa hapa nikajiuliza, jamani, hata hili la mzani wa kupimia watoto mpaka litoke MSD? Mganga wangu naomba hilo andiko la MSD ulifute, mimi kama Mbunge wenu nitaununua huo mzani, nimewasiliana na mtu wa famasi, ameniambia ndani ya wiki moja atakuwa ameuleta,” amesema Azza.

Credits:Nipashe

111 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital warts ni moja ya aina...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu Tatizo la...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

 PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake) PID NI NINI?  PID...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya kidonda mara moja. Mchakato huu...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa wa kuambukiza sana kwa watoto...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi mkubwa baada ya watoto wawili...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali kupitia chama chao cha wafanyakazi....

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya tumbaku yana athari kubwa kwa...

112
0