Stars Health
Mama Fatma Karume amefariki dunia,Septemba 21, 2026
Mama Fatma Karume amefariki dunia, Septemba 21, 2026.
Aliyekuwa Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume amefariki dunia, Septemba 21, 2026.
Taarifa ya kifo cha Bi.Fatma imetangazwa rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla ambapo amesema kimetokea Mbweni usiku huu.
Mama Fatma Karume alizaliwa Februari 2, 1929, Bumbwini Misufini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, na baadaye akaolewa na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambapo mbali na kuwa Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mama Fatma anatajwa kuwa miongoni mwa Wanawake walioshiriki katika harakati za kisiasa Zanzibar.
Mama Fatma pia ni Mama wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliyeiongoza Zanzibar kuanzia mwaka 2000 hadi 2010. Via@millardayo.
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)