Afya News
Hatari; Ongezeko kubwa la watu wanaogundulika kuwa na virusi vya HIV nchini Fiji
Hatari; Ongezeko kubwa la watu wanaogundulika kuwa na virusi vya HIV nchini Fiji
Serikali ya Fiji imetangaza dharura ya kitaifa ya HIV, kufuatia ongezeko kubwa la watu wanaogundulika kuwa na virusi vya HIV nchini humo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Huduma za Tiba ya Fiji, takwimu mpya zinaonyesha kuwa sasa takribani mtu mmoja kati ya kila watu wazima 60 anaishi na HIV, ikilinganishwa na mtu mmoja kati ya 167 miaka mitano iliyopita.
Takwimu rasmi za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa Fiji ilirekodi maambukizi mapya 2,016 mwaka 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 27 kutoka kesi 1,583 zilizoripotiwa mwaka 2024. Wizara imeeleza kuwa ongezeko hilo linaonyesha mchanganyiko wa maambukizi kuongezeka pamoja na kuimarika kwa upimaji na ufuatiliaji wa wagonjwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia HIV/AIDS (UNAIDS) linakadiria kuwa karibu watu 9,100 walikuwa wakiishi na HIV nchini Fiji mwaka 2025, huku asilimia 39 pekee wakijua hali zao za HIV na asilimia 22 wakiwa wanapata matibabu ya kupunguza makali ya virusi (ART).
Mamlaka za Fiji zimetangaza kuongeza upimaji wa HIV bila malipo, huduma za kinga ikiwemo PrEP, matibabu na mpango wa kutoa sindano na vifaa salama kwa watu wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga. UNAIDS imesema zaidi ya asilimia 42 ya visa ambavyo njia ya maambukizi ilijulikana vilihusishwa na matumizi ya dawa za kulevya kwa kujidunga, huku zaidi ya nusu vikihusishwa na maambukizi ya njia ya ngono.#KitengeUpdates
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)