Connect with us

Ebola

Tofauti ya virusi vya Bundibugyo (BDBV) na virusi vya Ebola

Avatar

Published

on

© WHO/Josua Mulala Raymond Ingawa virusi vya Bundibugyo vinasababisha ugonjwa wa Ebola, Bundibugyo si sawa na virusi vya Ebola vinavyojulikana kama EBOV.
211 Views
0 Comments

Virusi vya Bundibugyo (BDBV) ni mojawapo ya virusi vya familia ya Filoviridae vinavyoweza kusababisha ugonjwa wa Ebola. Mwaka 2026, virusi hivi vimesababisha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambao umesambaa hadi Uganda. Ingawa husababisha ugonjwa wa Ebola, Bundibugyo si sawa na virusi vya Ebola vinavyojulikana kama EBOV.

Bundibugyo ni nini?

Virusi vya Bundibugyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2007 katika wilaya ya Bundibugyo, magharibi mwa Uganda, baada ya kuzuka kwa homa ya kuvuja damu. Jina lake limetokana na eneo hilo.

Tangu kugunduliwa kwake, kumekuwa na milipuko mitatu:

  • 2007–2008 (Uganda)
  • 2012 (DRC)
  • 2026 (DRC na kusambaa hadi Uganda)

WHO inasema mlipuko wa mwaka 2026 ndiyo mkubwa zaidi kuwahi kurekodiwa.

Tofauti kati ya Bundibugyo na Ebola

Bundibugyo ni aina tofauti ya virusi vinavyoweza kusababisha ugonjwa wa Ebola. Virusi vya Ebola (EBOV) viligunduliwa mwaka 1976 karibu na Mto Ebola nchini DRC, wakati Bundibugyo viligunduliwa miaka 31 baadaye nchini Uganda.

Huambukizwaje?

Maambukizi yanaweza kutokea:

-Kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

-Kupitia mgusano wa moja kwa moja na damu au majimaji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa.

-Kupitia vitu vilivyochafuliwa na damu au majimaji ya mwili.

Wahudumu wa afya na walezi wako kwenye hatari kubwa zaidi ikiwa hawatazingatia hatua za kujikinga.

Dalili

Dalili za awali ni:

✓Homa

✓Uchovu mkubwa

✓Maumivu ya misuli

✓Maumivu ya kichwa

✓Maumivu ya koo

Kadiri ugonjwa unavyoendelea, mgonjwa anaweza kupata:

✓Kutapika

✓Kuharisha

✓Vipele

✓Matatizo ya figo na ini

✓Kutokwa na damu ndani au nje ya mwili

Vipimo vya maabara vinahitajika kuthibitisha maambukizi.

Kwa nini ni tishio?

Virusi vya familia ya Filoviridae vinaweza kusababisha milipuko mikubwa yenye vifo vingi. WHO inasisitiza umuhimu wa:

-Kugundua maambukizi mapema.

-Kuwahudumia wagonjwa haraka.

-Kufuatilia waliokutana na wagonjwa.

-Kuimarisha hatua za kuzuia maambukizi.

Kwa ujumla, ingawa Bundibugyo si maarufu kama virusi vya Ebola (EBOV), ni kirusi hatari kinachoweza kusababisha ugonjwa wa Ebola na kuleta tishio kubwa kwa afya ya umma ikiwa hakitadhibitiwa mapema.

References;

  1. World Health Organization. (2026, September 1). Ebola disease caused by Bundibugyo virus, Democratic Republic of the Congo and Uganda. World Health Organization. https://www.who.int/emergencies/disease-outbreak-news/item/2026-DON606
  2. United Nations. (2026, September 1). UDADAVUZI: Virusi vya Bundibugyo ni nini na vina tofauti gani na virusi vingine vinavyosababisha Ebola? UN News Kiswahili.
  3. Centers for Disease Control and Prevention. (2026). Ebola Disease Outbreak in the Democratic Republic of the Congo (HAN 00530). https://www.cdc.gov/han/php/notices/han00530.html
  4. Médecins Sans Frontières. (2026, May 20). The Bundibugyo virus challenge: Why is this Ebola disease outbreak different? https://www.msf.org/bundibugyo-virus-challenge-why-ebola-disease-outbreak-different
211 Views
0 Comments
✚

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital warts ni moja ya aina...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu Tatizo la...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

 PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake) PID NI NINI?  PID...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya kidonda mara moja. Mchakato huu...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa wa kuambukiza sana kwa watoto...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi mkubwa baada ya watoto wawili...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali kupitia chama chao cha wafanyakazi....

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya tumbaku yana athari kubwa kwa...

212
0