Afya News
Watu 800 waugua baada ya kula chakula cha bure
Watu 800 waugua baada ya kula chakula cha bure
Takribani watu 800 nchini Indonesia wameugua katika matukio tofauti yanayohusishwa na sumu ya chakula kilichotolewa kupitia mpango wa Serikali wa chakula cha bure. Kati yao, wanafunzi 512 waliugua baada ya kula chakula cha mchana Jumanne, Septemba 1, 2026, katika shule ya bweni ya Kiislamu iliyopo Sidoarjo.
Afisa wa Wakala wa Kitaifa wa Chakula nchini humo, Ketut Sumedana amesema jiko lililoandaa chakula hicho limesimamishwa kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ugonjwa huo. Kwa upande wake, Mbunge Charles Honoris amesema visa vingine vimeripotiwa Nganjuk, ambako watu 49 waliugua, na Agam, West Sumatra, ambako watu 237 wameathirika.
Akirejea takwimu kutoka idara za afya za maeneo hayo, Honoris amesema matukio hayo hayawezi kuchukuliwa kuwa ya bahati mbaya, akidai yanaashiria changamoto katika utekelezaji wa mpango huo. Mpango wa chakula cha bure ulianzishwa na Rais Prabowo Subianto mwaka 2025 kwa lengo la kupunguza utapiamlo nchini humo.Via#AzamTVUpdates
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa