Hospital
Hakuna kiwango chochote cha unywaji wa Pombe Salama kwa afya ya binadamu
Wananchi wametakiwa kuachana kabisa na matumizi ya pombe baada ya kubainika kuwa hakuna kiwango chochote cha unywaji kilicho salama kwa afya ya binadamu.
Wito huo umetolewa na Afisa Lishe Mwandamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala (MRRH), Bi. Gelagister Mwilike Gwarasa, alipokuwa akielezea athari za kilevi hicho katika afya na lishe ya binadamu, pamoja na mchango wake kwenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Bi. Gwarasa amesema kuwa tafiti za kitiba na miongozo ya kisayansi kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Wizara ya Afya nchini Tanzania, inaonesha wazi kuwa hakuna kiwango cha chini cha pombe kinachoweza kuitwa salama, kwani kiwango chochote kina mchango katika kusababisha madhara makubwa kiafya.
”Jamii yetu imezoea kutumia pombe kama kiburudisho, lakini bila kujali ni kiwango gani ambacho mtu anatumia, inashauriwa kitaalamu kwamba isitumike kwa sababu inaleta madhara,” alieleza Bi. Gwarasa.
Ameongeza kuwa, huko nyuma kulikuwa na miongozo iliyowekwa na WHO pamoja na Wizara ya Afya nchini iliyoruhusu matumizi ya kiwango kidogo cha pombe kwa wale ambao walishindwa kuacha kabisa, lakini msimamo wa sasa ni kwamba hakuna kiwango chochote kinachoruhusiwa, kwani ni hatari kwa afya ya mwili.
Credits:mwananyamalarrh
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)