Connect with us

Afya News

Hata Wanaume wanaweza Kuugua Saratani ya Matiti

Avatar

Published

on

Hata Wanaume wanaweza Kuugua Saratani ya Matiti

SARATANI ya matiti imeendelea kuwa changamoto ya kiafya inayohitaji elimu kwa jamii nzima, baada ya kubainika kuwa wanaume nao wanaweza kuugua ugonjwa huo, licha ya dhana iliyojengeka kuwa unawahusu wanawake pekee.

Kutokana na hali hiyo, wanaume wametakiwa kuacha dhana potofu na kuzingatia uchunguzi wa afya zao ili kubaini mapema viashiria vya ugonjwa huo na kupata matibabu kabla haujafikia hatua za juu.

Mkurugenzi wa Mradi wa Kuzuia Saratani ya Matiti na Mlango wa Kizazi kutoka Shirika la Jhpiego, Dk. Mary Rose, amesema takribani asilimia 2.5 ya wagonjwa wa saratani ya matiti ni wanaume, lakini wengi hawana mwamko wa kuchunguza afya zao.

Amesema ugonjwa huo unapogundulika mapema, uwezekano wa kupata matibabu yenye mafanikio huongezeka, hivyo ni muhimu kuimarisha elimu kwa jamii bila kujali jinsia.

“Wanaume nao wanapata saratani ya matiti, hivyo wanapaswa kuchunguza afya zao na kuwahi hospitalini wanapoona mabadiliko yasiyo ya kawaida,” amesema.

Katika hatua nyingine, Dk. Mary amesema kuanzia Januari mwakani kuna mpango wa kushirikiana na asasi ya kiraia kutoka India kuandaa mtaala wa kutengeneza matiti bandia kwa njia rahisi, pamoja na kuwajengea uwezo wanawake wanaoishi na saratani ya matiti.

Amesema mpango huo unalenga kuwasaidia wanawake waliokatwa matiti kurejesha hali ya kujiamini na kuongeza upatikanaji wa matiti bandia.

Naye, Msaidizi Meneja wa Kitengo cha Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar, Zuhura Saleh Amour, amesema wanawake 229 waliokatwa matiti kutokana na saratani wamepatiwa matiti bandia ili kuwasaidia kukabiliana na mabadiliko ya miili yao baada ya upasuaji.

Amesema huduma hiyo ni muhimu katika kurejesha hali ya kujiamini na kupunguza unyanyapaa, huku akihimiza jamii kuwaunga mkono wanawake hao ili waendelee kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, wagonjwa 115 walithibitishwa kuwa na saratani ya matiti katika mwaka wa 2025/2026, huku asilimia 58 wakigundulika katika hatua ya tatu na ya nne.

Takwimu hizo zinaonesha umuhimu wa kuimarisha elimu na uchunguzi wa mapema ili kupunguza madhara ya ugonjwa huo, hasa kwa wagonjwa wanaochelewa kutafuta huduma za afya.Via #IPP Media.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

Utafiti23 hours ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...