Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

Hospital

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Avatar

Published

on

Daktari Bingwa Bobezi wa Magonjwa ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka hospitalini hapo, Dk Brighton Mushengezi.
253 Views
0 Comments

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo hilo na umuhimu wa jamii kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huo.

Daktari Bingwa Bobezi wa Magonjwa ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka hospitalini hapo, Dk Brighton Mushengezi, amesema kiharusi kinaendelea kuwa changamoto kubwa ya kiafya duniani na hutokea pale mzunguko wa damu kwenda kwenye ubongo unapozuiwa au mshipa wa damu katika ubongo unapopasuka.

Amesema hali hiyo husababisha sehemu ya ubongo kukosa oksijeni na virutubisho vinavyohitajika, jambo linaloweza kusababisha madhara makubwa kwa mgonjwa endapo hatapatiwa huduma kwa wakati.

Kwa mujibu wa Dk Mushengezi, dalili za kiharusi zinaweza kujitokeza ghafla na ni pamoja na uso kupinda upande mmoja, mkono au mguu kuwa dhaifu au kufa ganzi, kushindwa kuzungumza au kuelewa mazungumzo, kupoteza uwezo wa kuona pamoja na kushindwa kutembea vizuri.

Amesema takwimu za Shirika la Kiharusi Duniani (World Stroke Organization) za mwaka 2025 zinaonesha kuwa takribani watu milioni 12 hupata kiharusi kila mwaka duniani.

Ameongeza kuwa shirika hilo linaeleza pia kuwa mtu mmoja kati ya watu wanne wenye umri wa miaka 25 na kuendelea yuko katika hatari ya kupata kiharusi katika maisha yake, hali inayosisitiza umuhimu wa jamii kuwa na uelewa wa ugonjwa huo na kuchukua hatua za kinga. Via #HabarileoUPDATES

253 Views
0 Comments
✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

Stars Health5 hours ago

Hali ya Papa Leo XIV imeendelea kuimarika baada ya upasuaji wa mapafu

Papa Leo XIV anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye pafu. Vatican yasema alikuwa na usiku mtulivu...

Ebola8 hours ago

Kenya yathibitisha mgonjwa wa pili wa Ebola,ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo

Kenya imethibitisha kisa cha pili cha ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo, huku mamlaka za afya zikieleza kuwa mgonjwa huyo...

Afya News9 hours ago

Vifo vya Wajawazito barani Afrika mada hii imeibuka tena

Tatizo la wajawazito kupoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, limetajwa katika mkutano wa kanda wa kuimarisha...

Stars Health14 hours ago

Upasuaji wa Papa umefanikiwa,baada ya kugunduliwa Saratani ya mapafu

Papa Leo XIV aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu lakini alifanyiwa upasuaji uliofanikiwa kuondoa sehemu ya chini ya pafu lake...

magonjwa2 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na...

WHO2 days ago

Kifo cha mfanyakazi wa maabara NCHINI URUSI chazua maswali kuhusu NIMONIA isiyojulikana chanzo chake

Kifo cha mfanyakazi wa maabara NCHINI URUSI chazua maswali kuhusu NIMONIA isiyojulikana chanzo chake Tarehe ya kuchapishwa: 13 Oktoba 2026...

EVENTS2 days ago

Mwanaume Afariki Baada ya Kuanguka Kutoka Kwenye Mchezo wa Roller Coaster wa Urefu wa Takribani Mita 61 Nchini Marekani

Mwanaume Afariki Baada ya Kuanguka Kutoka Kwenye Mchezo wa Roller Coaster wa Urefu wa Takribani Mita 61 Nchini Marekani Tarehe...

afyatips2 days ago

Jinsi ya kuongeza damu kwa haraka

Jinsi ya kuongeza damu kwa haraka Chembe hai nyekundu za damu maarufu kama Haemoglobin(hb) ndizo hutumika katika kuangalia kiwango cha...

magonjwa ya Zinaa6 days ago

Ugonjwa wa Genital herpes,chanzo,dalili na Tiba

HERPES SEHEMU ZA SIRI: DALILI, NAMNA INAVYOAMBUKIZWA, KINGA NA MATIBABU Herpes sehemu za siri (Genital herpes) ni maambukizi ya zinaa...

Afya News3 days ago

Vipimo vya Vinasaba kutumika kutambua waliofariki kwa Ajali Morogoro

Vipimo vya Vinasaba kutumika kutambua waliofariki kwa Ajali Morogoro Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, amewataka ndugu wa watu...

254
0