Connect with us

Afya News

Sera za likizo ya uzazi yenye malipo kwa akina baba

Avatar

Published

on

ILO Tangu ILO ianzishwe mwaka 1919, viwango vya ajira vimekuwa vinazingatiwa ikiwemo likizo ya uzazi kwa wanawake wajawazito ambao wanafanya kazi.

Sera za likizo ya uzazi yenye malipo katika sehemu nyingi duniani zinawapa akina mama muda mrefu zaidi wa kulea watoto kuliko akina baba, hali inayochangia kutokuwiana kwa majukumu ya malezi na kuathiri familia, watoto na uchumi.

Hayo ni kwa mujibu wa muhtasari mpya wa sera wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women) na mradi wa Kundi la Benki ya Dunia wa Wanawake, Biashara na Sheria.
Katika nchi na maeneo 190 yaliyofanyiwa utafiti, 61 hayafikii kiwango cha Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa Duniani ILO, cha wiki 14 za likizo yenye malipo kwa akina mama, huku sita hazihakikishi likizo hiyo. Kwa upande wa akina baba, nchi na maeneo 66 hazihakikishi likizo ya uzazi yenye malipo.

Kati ya 124 zinazotoa likizo hiyo kwa akina baba, nusu hutoa chini ya wiki mbili. Kwa wastani, akina mama wanastahili likizo ya uzazi yenye malipo iliyo karibu mara nane ya wanayopata akina baba, kwa mujibu wa takwimu za Wanawake, Biashara na Sheria.
Mwanamke aliyevaa shati la njano akiwa amembeba mtoto mchanga katika chumba cha hospitali nchini Liberia.
Benki ya Dunia/Dominic Chavez Ripoti ILO inasema kwamba likizo ya uzazi yenye malipo au ulinzi wa uzazi ni haki ya binadamu na ajira kwa wote.
Likizo za malipo muhimu kwa kina baba katika malezi
Licha ya wanaume wengi kutaka kushiriki zaidi katika malezi, asilimia 87 ya akina baba wanasema hawapati msaada wanaohitaji, huku asilimia 83 wakisema waajiri wao hawatoi mipango ya kazi inayoweza kubadilika. Zaidi ya asilimia 64 wanaunga mkono ongezeko la kodi ili kupanua huduma za malezi za umma, kwa mujibu wa utafiti kuhusu hali ya akina baba duniani wa mwaka 2026.
“Malezi yanasaidia familia, jamii na uchumi wetu, lakini wanawake bado wanabeba sehemu kubwa isiyo na uwiano ya jukumu hili,” amesema Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women, Nyaradzayi Gumbonzvanda.

Akina baba wanapochukua likizo, hushiriki zaidi katika malezi ya watoto na kazi za nyumbani hata baada ya kurejea kazini, na hivyo kupunguza mzigo kwa wanawake.

Kwa wastani, wanawake hutumia muda ulio mara 2.5 zaidi ya wanaume katika kazi za malezi zisizolipwa, kwa mujibu wa ripoti ya UN Women kuhusu pengo la kijinsia. Likizo ya akina baba pia inahusishwa na ongezeko la kipato cha akina mama na ushiriki wao katika ajira, huku watoto wakinufaika na ushiriki mkubwa wa baba katika malezi.
Takribani mzazi mmoja kati ya wanne huwalea watoto na pia kuwahudumia watu wazima wenye umri mkubwa. UN Women na Kundi la Benki ya Dunia zinatoa wito wa kuimarisha mifumo ya malezi kupitia likizo zenye malipo, huduma za malezi na ulinzi wa kijamii ili majukumu yagawanywe kwa usawa.

Credits:UN

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

Utafiti1 day ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...