Connect with us

Afya News

TACAIDS yaongeza kasi ya utekelezaji wa hatua za kinga, upimaji na matibabu ya Virusi vya Ukimwi (VVU)

Avatar

Published

on

TACAIDS yaongeza kasi ya utekelezaji wa hatua za kinga, upimaji na matibabu ya Virusi vya Ukimwi (VVU)

Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), imeongeza kasi ya utekelezaji wa hatua za kinga, upimaji na matibabu ya Virusi vya Ukimwi (VVU), ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutokomeza UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza, jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema Tanzania inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kudhibiti VVU na UKIMWI, ikiwemo kufufua kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI), kilichopo mkoani Arusha, kinachozalisha dawa za kufubaza makali ya VVU.

Profesa Kabudi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, TACAIDS, Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA), Serikali za Mitaa, asasi za kiraia, sekta binafsi, washirika wa maendeleo na jamii katika kuongeza uelewa, kupunguza unyanyapaa na kuhakikisha huduma za kinga na matibabu zinawafikia vijana, wanawake na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho, amesema Tanzania imepiga hatua katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU na vifo vinavyotokana na UKIMWI, huku Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Deogratius Rutatwa, akiishukuru Serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za matibabu na dawa za kinga zinazowasaidia watu wanaoishi na VVU kuishi kwa kujiamini.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti24 hours ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...