Ukimwi
Unaweza kupima Ukimwi Kipimo kikaonyesha Unao lakini huna
HIV false positive test maana yake ni nini?
HIV false positive test maana yake ni mtu kupata majibu ya kipimo cha VVU yanayoonyesha kuwa ana VVU, wakati kiuhalisia hana maambukizi ya VVU.
Kwa Kiswahili, hali hii huitwa majibu chanya ya uongo ya kipimo cha VVU.
Hii Inatokeaje?
Mtu anaweza kupata majibu ya false positive kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo:
(1)Hitilafu ya kipimo: Kipimo kinaweza kutoa majibu yasiyo sahihi.
(2)Makosa ya maabara: Kwa mfano, kuchanganya sampuli za damu au kutafsiri matokeo kimakosa.
(3)Hali fulani za kiafya: Baadhi ya magonjwa au hali za kinga ya mwili zinaweza kuathiri matokeo ya vipimo fulani.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaMwitikio usiohusiana moja kwa moja na VVU: Wakati mwingine, kingamwili au vitu vingine mwilini vinaweza kuathiri kipimo na kusababisha majibu chanya ya uongo.
NB: Ndyo mana pia,Kupima kipimo kimoja cha Rapid Test haitoshi, ni muhimu kufanya na UNIGOLD TEST.
Je, mtu akipima HIV positive, ina maana ana VVU?
Si lazima kipimo kimoja chanya kiwe uthibitisho wa mwisho wa maambukizi ya VVU.
Mtu anapopata majibu chanya, anapaswa kufuata utaratibu rasmi wa upimaji wa VVU unaotumika nchini Tanzania ili kuthibitisha hali yake. Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza kutumia mkakati wa vipimo vitatu ili kupunguza uwezekano wa kutoa utambuzi usio sahihi.
Mtu afanye nini akipata majibu ya HIV false positive?
Asiwe na hofu wala kuhitimisha kuwa ana VVU kutokana na kipimo kimoja pekee.
Aende kituo cha afya kilichoidhinishwa kwa ushauri na upimaji zaidi.
Afuate maelekezo ya mhudumu wa afya kuhusu vipimo vya kuthibitisha hali yake.
Asianze au kuacha dawa za VVU bila ushauri wa mtaalamu wa afya.
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

