Amoxicillin inatibu ugonjwa gani
Katika makala hii tumechambua baadhi ya magonjwa ambayo hutibiwa kwa kutumia dawa aina hii ya Amoxicillin
1. Ijue dawa ya amoxicillin inatibu nini
Amoxicillin ni dawa ambayo ipo kwenye kundi la penicillin antibiotic. Dawa hii inaweza kutumika kutibu maambukizi mbali mbali ya bacteria(bacterial infections),
Maambukizi hayo ni pamoja na; Maambukizi ya kifua/chest infections ikiwemo ugonjwa wa pneumonia, majibu kwenye meno(dental abscesses).
Dawa hii huweza kutumika pamoja na aina nyingine za antibiotics kutibu magonjwa mengine mengi.
Dawa ya Amoxicillin huweza kutumika kutibu maambukizi ya Sikio pamoja na maambukizi ya kifua kwa Watoto, Hiyo ni kwa Uchache tu ila;
Amoxicillin hutumiwa kutibu aina nyingi za maambukizi ya bakteria. Dawa hii ni antibiotic,aina ya penicillin. Hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria, Antibiotic hii hutibu maambukizi ya bakteria pekee.
Haitafanya kazi kwa maambukizi ya virusi (haiwezi kutibu magonjwa yanayotokana na maambukizi ya Virusi).
Kutumia antibiotiki yoyote wakati haihitajiki kunaweza kusababisha isifanye kazi kwa maambukizi ya siku zijazo.Amoxicillin pia hutumiwa pamoja na dawa nyingine kutibu vidonda vya tumbo/utumbo vinavyosababishwa na bakteria H. pylori na kuzuia vidonda kurudi.
Dawa ya Amoxicillin huja kwa mfumo wa;
- vidonge(capsules),
- Maji au syrup,
- pia huweza kutolewa kama Sindano.
2. Mambo muhimu ya kufahamu kuhusu dawa ya amoxicillin
– Kwa asilimia kubwa,maudhi madogo madogo au Side effects ya dawa hii ya amoxicillin ni kuhisi kichefuchefu pamoja na kuharisha
– Aina ya amoxicillin inayokuja kwa mfumo wa maji au syrup huweza kutia doa kwenye meno yako(stain your teeth).
Uzuri ni kwamba madoa haya hayadumu, huweza kuondolewa mara moja kwa kupiga tu mswaki.
– Usitumie dawa hii pasipo kupewa maelekezo ya kitaalam.
3. Nani anaruhusiwa kutumia na nani haruhusiwi kutumia dawa ya amoxicillin
Dawa hii ya amoxicillin huweza kutumiwa na Watu wazima pamoja na watoto, ingawa sio salama kwako ikiwa;
• Una mzio au unapata allergic reaction unapotumia dawa hii ya amoxicillin au dawa zingine zote jamii ya penicillin
• Usitumie amoxicillin ikiwa una matatizo ya Ini au Figo,
• Ndyo umepewa saivi chanjo yoyote, au umepewa hivi karibuni chanjo yoyote.n.k
4. Matumizi ya dawa ya amoxicillin(Dosage)
Kiwango cha kawaida cha vidonge vya amoxicillin(capsules) ni 250mg hadi 500mg, Na huweza kutumika mara 3 kwa siku. Lakini Kiwango hiki kinaweza kupunguzwa zaidi kwa watoto.
Syrup/Kioevu au kimiminika cha Amoxicillin kinapatikana katika kipimo cha 125mg na 250mg.
Muhimu:
Endelea kutumia dawa hii hadi ukamilishe dozi hiyo, hata kama unahisi nafuu. Ukiacha matibabu yako mapema, maambukizi yanaweza kurudi tena.
Jinsi ya kutumia:
Ikiwa unatumia mara 3 kwa siku, hii inaweza kuwa asubuhi, katikati ya mchana na wakati wa kulala.
Kumbuka; Kutwa mara 3-Ni kila baada ya masaa 8. Soma vizuri hapa Saa za kumeza dawa
Unaweza kutumia dawa ya amoxicillin kabla au baada ya chakula,Meza vidonge vya amoxicillin vikiwa vizima kwa kunywa maji. Usivitafune au kuvivunja.
Amoxicillin inapatikana kama Syrup kwa watoto na watu ambao wanaona vigumu kumeza vidonge.
Ikiwa wewe au mtoto wako mnatumia amoksilini syrup, kwa kawaida itatengenezewa kwa ajili yako. Dawa itakuja na kizibo cha plastiki au kijiko ili kukusaidia kupima kipimo sahihi. Ikiwa haina, muulize mfamasia wako. Usitumie kijiko cha jikoni kwani hakitapima kiwango sahihi.