SALMONELLA TYPHI BACTERIA ANAYESABABISHA UGONJWA WA TYPHOID(HOMA YA MATUMBO)
Salmonella Typhi ambapo mara nyingi huandikwa kwa kifupi kama S.Typhi,ni bacteria ambaye hushambulia sehemu ya utumbo pamoja na damu,
Bacteria huyu ndiye husababisha ugonjwa wa homa ya matumbo kwa kitaalam Typhoid Fever.
Kwa asilimia kubwa watu hushambuliwa na bacteria hawa na kupata ugonjwa wa Typhoid baada ya kunywa maji machafu,
Maji ambayo yana uchafu wa kila namna ikiwemo vinyesi vya binadamu. Maji ambayo hayajatibiwa,maji ambao sio safi na salama.
BAADHI YA DALILI BAADA YA MTU KUSHAMBULIWA NA BACTERIA HAWA,
Hizi hapa chini ni dalili za awali kabsa baada ya mtu kushambuliwa na Salmonella Typhi kisha kupata Ugonjwa wa Typhoid au homa ya matumbo.
- Joto la mwili kuwa juu sana hata kuweza kufikia 40.5 C au mtu kuwa na homa
- Mtu kupata maumivu makali sana ya kichwa
- Mwili kuchoka sana kuliko kawaida na kuwa dhaifu sana
- Kupata maumivu kwenye misuli ya mwili
- Mwili Kutoa jasho sana
- Wengine kuanza kupata kikohozi kikavu sana yaani dry cough
- Hamu ya chakula kupotea kabsa au mtu kukosa hamu ya kula chochote
- Kupata maumivu ya tumbo
- Uzito wa mwili kuanza kupungua
- Tumbo kuanza kuvimba na kuwa kubwa zaidi
- Kupata tatizo la Kuharisha,
- Mwili kuanza kuwa na rashes
- Na wengine kuanza kupata shida ya choo kigumu yaani constipation n.k
KUMBUKA;Ukiona dalili kama hizi,hakikisha unapata msaada wa haraka kutoka kwa wataalam wa afya,
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.