Chadema; hakuna watu wanaathirika kwenye hoja ya afya kuliko wamama
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kutoa tamko kuhusiana na Bima ya Afya nchini kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kufanyika Machi 8, 2024.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara kupitia kikao cha ndani, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema chama kitaadhimisha rasmi siku hiyo jijini humo na kutoa tamko hilo.
Kikao hicho kimefanyika leo Machi 6, 2024 na kukutanisha viongozi wa chama hicho kutoka majimbo mbalimbali katika Mkoa huo.
“Siku ya tarehe 8, mwezi huu ni Siku ya Wanawake Duniani na hakuna watu wanaathirika kwenye hoja ya afya kuliko wamama, kwasababu wana mambo mengi yanayohitaji masuala ya bima ikiwemo uzazi”
“Na kila kitu na ndiyo wanao tunza watoto, wababa tunayajua haya lakini hatuyajuwi kama wamama.’’amesema Mbowe
Amesema katika hatua ya sasa wameiomba serikali kuwasikiliza watoa huduma hiyo ili wananchi wapate huduma bora inayokidhi matibabu ya wagonjwa, Watanzania wanaofikwa na mahiatji ya matibabu.
Akijibu maswali ya baadhi na waandishi hao likiwemo juu ya swala zima la kugawa majimbo ya uchaguzi nchini, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu amesema kwa mujibu wa katiba ya nchi ya mwaka 1977.
‘’Unapotenga majimbo ya uchaguzi, tume itaangalia usawa wa idadi ya watu’’