KUVIMBA MASHAVU YA UKE
• • • • • •
Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu ya Uke,Dalili pamoja na Matibabu yake.
Je umeshangaa tu ukijichunguza sehemu zako za Siri kuna kitu kama kimevimba Ukeni? je ni nini hiki?
SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)
Hali ya kawaida ya uke au sehemu za siri za mwanamke ni ya unyevu unyevu,
Endapo kuna ukavu hicho ni kiashiria mojawapo kwamba kuna tatizo.
Ifahamike kwamba lipo tezi maalum kwa ajili ya kazi hiyo ya kuleta hali ya unyevu unyevu, au ute ukeni na tezi hilo huitwa Bartholin.
Sasa endapo kutatokea shida kwenye vimirija vidogo vya tezi hili la Bartholin Mfano kuziba N.K
huweza kusababisha yale maji yanayozalishwa na tezi hili kwa ajili ya kuleta hali ya Unyevu unyevu ukeni,
kujaa na hivo kusababisha mashavu ya Uke kuvimba, Hali hii kwa kitaalam huitwa Bartholin Cyst.
Hali ya kuziba vimirija hivi huweza kuhusishwa na sababu ambazo sio za moja kwa moja,
Mfano maambukizi ya magonjwa mbali mbali hasa ya zinaaa kama Kisonono N.k.
DALILI ZA TATIZO HILI LA kuvimba mashavu ya Uke
Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za tatizo la kuvimba mashavu ya Uke;
– Kuanza kupata maumivu wakati unafanya mapenzi
– Kupata maumivu wakati wa kutembea
– Shavu la Uke Kuvimba,
Shavu la uke upande uliothirika na shida hii Kuvimba
– Kupatwa na dalili zingine kama joto la mwili kupanda au kuwa na homa
– Kuanza Kutokwa na uchafu ukeni
– Kusikia au kuhisi ule uvimbe wakati wa kutembea n.k
MATIBABU ya tatizo hili la kuvimba mashavu ya Uke
Kama nilivyokwisha kusema hapo awali kuvimba mashavu ya Uke kunasababishwa na sababu mbali mbali,
Hivo kabla ya kuanza Tiba yoyote ni muhimu zaidi kuongea na wataalam wa afya ili kujua chanzo halisi ni nini,ndipo uanze matibabu yake.
• zipo tiba kadhaa ambazo unaweza kupata hospital kulingana na hali yako na ukawa sawa kabsa, na tiba hizo ni kama vile;
- Upasuaji
- au kutumbua sehemu ya Uvimbe
- Pamoja na Dawa,
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Hitimisho
Ni muhimu sana kufahamu kuhusu dalili za tatizo la kuvimba mashavu ya Uke ili ukiona hali ya tofauti upate msaada wa matibabu,
Dalili za tatizo la kuvimba mashavu ya Uke ni pamoja na;
– Kuanza kupata maumivu wakati unafanya mapenzi
– Kupata maumivu wakati wa kutembea
– Shavu la Uke Kuvimba,
Shavu la uke upande uliothirika na shida hii Kuvimba
– Kupatwa na dalili zingine kama joto la mwili kupanda au kuwa na homa
– Kuanza Kutokwa na uchafu ukeni
– Kusikia au kuhisi ule uvimbe wakati wa kutembea n.k