Chuchu kutoa maji ni dalili ya nini
Chuchu kutoa Maji linaweza kuwa tatizo la kawaida,Ingawa wakati mwingine huweza kuwa dalili mbaya Zaidi. Ni muhimu sana kuongea na Wataalam wa afya ikiwa una dalili hii ili kujua nini kinaendelea mwilini.
Pia Kama una shida hii tunaweza kuwasiliana hapa ndani ya @afyaclass, #SOMA pia chuchu kutoa Maziwa yenyewe wakati Sio mjamzito wala hunyonyeshi.
Fahamu,chuchu kutoa maji huweza kutokea kwa asilimia 80% ya watu ambao wapo kwenye umri wa kuzaa, hata kama sio wajawazito au kunyonyesha,
Kila titi lina takribani mirija(ducts) 20 ya maziwa, na maji huweza kutokea hapo pia,Ni kawaida maziwa au maji maji kutoka yenyewe ikiwa una mimba au kunyonyesha.
Dalili Zingine:
Dalili Zingine ambazo huweza kuambatana na chuchu kutoa Maji ni pamoja na;
– Kupata Maumivu ya titi au chuchu
– Kuvimba kwa titi au Uvimbe kuzunguka chuchu
– Kubadilika kwa chuchu mfano;
- Chuchu kuingia ndani
- chuchu kubadilika rangi
- Chuchu kuwasha
- Chuchu kutoa magamba
- Chuchu kuwa na Vidonda n.k
– Mabadiliko ya ngozi ya titi, ikiwemo; titi kuwa jekundu, kupata vipele au rashes,vidonda n.k
– Kubadilika kwa size au Umbo la Titi,mfano titi moja kuwa kubwa kuliko lingine n.k
– Kupata Homa
– Kuhisi kichefuchefu na Kutapika
– Kukosa Hedhi au periods
– Mwili kuchoka sana kupita kiasi n.k
Utokwaji huo wa Maji kwenye chuchu unaweza kutoka kwa chuchu moja au zote mbili. Chuchu Inaweza kuvuja yenyewe au ukiibana/kuiminya,
Ingawa baadhi ya Tafiti zinasema, sio wazo nzuri kuiminya chuchu. Hii inaweza kufanya hali yoyote ya msingi ambayo haijatambuliwa kuwa mbaya zaidi. Ikiwa utaiacha peke yake, kutokwa na maji kunaweza kuacha peke yake.
Chanzo cha Chuchu kutoa maji
Unapokuwa mjamzito au kunyonyesha, kiasi kidogo cha maziwa kinaweza kuvuja. Kuvuja kunaweza kuanza mapema katika kipindi cha ujauzito wako, na unaweza kuendelea kuona maziwa hadi miaka 2 au 3 baada ya kuacha kunyonyesha.
Walakini, unaweza kutokwa na Maji hata kama wewe si mjamzito au kunyonyesha. Sababu zingine za kutokwa na maji kwenye chuchu ni pamoja na:
1. Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango,Mfano; Vidonge vya Uzazi wa mpango(birth control pills)
2. Maambukizi kwenye titi au Titi kuwa na jipu
3. Kuwa na tatizo la duct papilloma, ukuaji usio na madhara kama wart katika mirija ya matiti yako
4. Matumizi ya baadhi ya Dawa, Mfano dawa zinazoongeza kiwango cha vichocheo vinavyozalisha maziwa kama vile Prolactin,
Mfano ni dawa jamii ya antidepressants pamoja na ranquilizers
5. Kusisimua matiti au chuchu kupita kiasi
6. Kuwa na tatizo la fibrocystic breasts
7. Mabadiliko ya Vichocheo mwilini, ikiwemo kipindi cha Hedhi au Ukomo wa Hedhi(menopause)
8. Kuumia au kupata Majeraha kwenye matiti
9. Kuwa na tatizo la kuziba kwa mirija ya maziwa yaani kwa kitaalam
mammary duct ectasia,
10. Kuwa na Uvimbe usio Saratani kwenye tezi la pituitary(prolactinoma)
11. Tatizo la Tezi la Thyroid kutokufanya kazi vizuri yaani underactive thyroid gland
12. Kuwa na Saratani ya matiti(breast cancer) n.k
Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya mapema ikiwa una tatizo hili la Chuchu Kutoa Maji au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.