Dalili za Ukimwi ukeni,Soma hapa kufahamu
Zipo dalili mbali mbali ambazo huweza kujitokeza kwa mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU), lakini leo tunazungumzia baadhi ya Dalili hizo kwa Mwanamke.
Kumbuka; Sio kila Mwanamke Mwenye Dalili hizi tayari ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU), Dalili hizi huweza kuingiliana kwa kiasi kikubwa na magonjwa Mengine..
#SOMA pia; Dalili za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kwa UJUMLA
Dalili za Ukimwi kwa Mwanamke
Hizi hapa ni baadhi ya Dalili hizo kwa Mwanamke; (Info via|”HIV symptoms in women include:https://www.verywellhealth.com/hiv-symptoms-in-women-5095870
1. Kupata maambukizi ya fangasi Ukeni mara kwa mara,
Hali hii huweza kutokea kwa Sababu ya kuchuka kwa kinga ya mwili kutokana na maambukizi ya VVU,
Hii hufanya iwe rahisi mwili wako kushambuliwa na magonjwa mengine kwa urahisi Zaidi.
2. Kuwa na Vidonda Ukeni(Vaginal soreness)
3. Kuhisi hali ya Kuungua Ukeni(Vaginal burning)
4. Kupata Vipele Ukeni
5. Kupata Malengelenge Ukeni
6. Hedhi kuanza kuvurugika(Irregular periods)
7. Mwanamke kupata maumivu kwenye eneo la nyonga, au pelvis
8. Mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo
9. Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa
10. Damu kuvuja Ukeni, au kupata hedhi katikati ya mwezi
11. Kutoa damu kama vidoa vidoa
12. Kuvuja damu nyingi Ukeni
13. Kutokwa na Uchafu kama maji,uliochanganyika na damu na pia kuna muda unakuwa na harufu.
Dalili za HIV/AIDS kwa wanawake zinaweza kutofautiana kulingana na hatua ya maambukizi na jinsi mwili wa mtu unavyoendelea kuathirika.
Baadhi ya dalili zinazoweza kuashiria uwezekano wa kupata maambukizi ya HIV/AIDS kwa wanawake ni pamoja na maambukizi ya mara kwa mara ya magonjwa ya zinaa, maumivu au kuwashwa ukeni, kutokwa na ute mzito usio wa kawaida, kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa, na kuwa na uvimbe au maumivu katika sehemu za siri.
Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba dalili hizi zinaweza kuwa za magonjwa mengine na si lazima ziwe dalili za HIV/AIDS pekee. Ili kuthibitisha hali yako, ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu na kupimwa virusi vya HIV.