Dalili za kupevusha mayai,Soma hapa
Kupevusha mayai; ni pale ambapo mayai yamekomaa na sasa yanatoka kwenye vifuko vyake vya mayai(ovaries),
Hatua hii kwenye mzunguko wa hedhi hujulikana kama”Ovulation” . Mara yai linapotoka kwenye ovari, husafiri kupitia mrija wako wa fallopian ambapo husubiri kutungishwa na shahawa/mbegu za kiume. Kwa wastani, hufanyika siku ya 14 kwenye mzunguko wa hedhi wa Siku 28.”
Dalili za kupevusha mayai
Dalili za kupevusha mayai (ovulation) kwa wanawake zinaweza kujumuisha mambo kama vile:
1. Kutokwa na ute ute unaovutika kama ule wa Yai,
Hii ni dalili mojawapo kubwa ya kwamba Mwanamke yupo kwenye kipindi cha Siku za hatari au siku za kupevushwa kwa mayai(Ovulation).
2. Kutokwa na majimaji ya ukeni yenye ute mzito:
Mara nyingi, mwanamke anaweza kugundua ute mwingi, wenye kuvutika na laini kama vile yai. Hii inaweza kuwa dalili ya kupevusha mayai.
Kumbuka; Ute huu hautakiwi kuwa na harufu mbaya pamoja na rangi isiyoyakawaida. Ukiona hivi, hii huweza kuwa dalili ya maambukizi mengine(infections).
Soma Zaidi hapa aina ya Ute ukeni,rangi zake na maana zake
3. Kuongezeka kwa hamu ya tendo la ndoa:
Baadhi ya wanawake wanaweza kuhisi hamu kubwa ya tendo wakati wa kipindi cha ovulation. Hii inatokana na mabadiliko ya homoni ambayo huambatana na mchakato huu.
4. Maumivu ya tumbo chini:
Baadhi ya wanawake wanaweza kuhisi maumivu ya muda mfupi au ya kubana kwenye tumbo la chini. Hii inaitwa “maumivu ya ovulation” na mara nyingi hutokea upande mmoja wa tumbo.
5. Kuongezeka kwa hisia za harufu:
Baadhi ya wanawake wanaweza kuhisi hisia kali za harufu wakati wa ovulation. Hii inaweza kuwa mojawapo ya ishara za mwili kuelekea kipindi cha ovulation.
6. Mabadiliko ya joto la mwili:
Baadhi ya wanawake hurekodi mabadiliko ya joto la mwili wakati wa ovulation. Mara nyingi, joto la mwili huongezeka kidogo baada ya ovulation kutokana na ongezeko la homoni ya progesterone.
7. Mabadiliko ya hisia:
Baadhi ya wanawake wanaweza kuhisi mabadiliko ya hisia wakati wa ovulation, kama vile kuwa na hisia za furaha au hisia zingine.
Kumbuka kuwa kila mwanamke ni tofauti, na dalili hizi zinaweza kutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Ni muhimu kufuatilia mabadiliko katika mwili wako na kujifunza jinsi mwili wako unavyoonyesha ishara za ovulation ili uweze kutambua wakati unapokuwa unapevusha mayai.
KUPEVUSHWA KWA YAI au Ovulation(Kwa Wanawake)
Kupevushwa kwa yai, ni pale ambapo yai hutoka kwenye vifuko vya mayai yaani Ovaries na kuingia kwenye mirija ya uzazi ambayo hujulikana kwa kitaalam kama fallopian tubes, kitendo hiki ndyo kinaitwa OVULATION.
FAHAMU BAADHI YA MAMBO KUHUSU UPEVUSHAJI WA MAYAI AU OVULATION
1. Upevushaji wa mayai huhusiana na yai kutoka kwenye vifuko(ovaries) vyake kwenda kwenye mirija ya uzazi
2. Upevushaji wa mayai au Ovulation hutokea siku ya 14 kwa Wanawake wenye mzunguko wa siku 28
3. Ili mwanamke apate mimba lazima upevushaji wa mayai utokee
4. Kuna baadhi ya wanawake wenye matatizo ya mayai kutokupevushwa kabsa au kutokupevushwa kwa wakati
5. Mwanamke huweza kupevusha mayai mawili kwa wakati mmoja yaani kutoka ovary ya kulia na kushoto japo ni mara chache kutokea, hapa ndipo mapacha wasio Fanana huweza kupatikana yaani Fraternal twins baada ya urutubishaji wa mayai yote mawili
6. Baada ya mayai kutoka kwenye vifuko vyake(ovaries) huingia kwenye mirija ya uzazi yaani fallopian tubes, Na endapo mwanamke akafanya mapenzi na mwanaume kipindi hiki huweza kupata ujauzito
7. Kama urutubishaji wa yai umeshatokea,moja kwa moja kiumbe huenda kujishikiza kwenye kuta za mji wa mimba kitendo ambacho hujulikana kama Implantation na kuendelea kukua mpaka mtoto azaliwe,
8. Na kama urutubishaji haukutokea basi yai lile huharibika na kutoka kwa Njia ya HEDHI au period.
kumbuka; Ikiwa una tatizo Lolote kwenye mzunguko wako wa hedhi, hakikisha unapata Msaada au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.