Dalili za nyongo kuzidi mwilini
Katika Makala hii tumechambua dalili za nyongo kuzidi mwilini pamoja na tatizo la bile reflux, soma hapa Zaidi..!!!
Nyongo ni nini?
Nyongo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Bile ni kimiminika cha rangi ya kijani (physiological aqueous solution) ambacho huzalishwa na Ini. Na vitu vinavyopatikana kwenye nyongo ni pamoja na;
- bile salts,
- phospholipids,
- cholesterol,
- conjugated bilirubin,
- electrolytes,
- Pamoja na maji(water) .
Nyongo huzalishwa na ini na kuhifadhiwa katika kibofu cha nyongo kabla ya kutolewa mwilini kusaidia katika mmeng’enyo wa mafuta. Nyongo husaidia kuvunja mafuta mwilini ili kuyafanya yaweze kusagika na kufyonzwa na mwili.
Hata hivyo, kuna hali ambazo zinaweza kusababisha matatizo katika uzalishaji, kutolewa, au kumeng’enywa kwa nyongo, na hii inaweza kusababisha dalili za nyongo kuzidi mwilini.
Dalili za nyongo kuzidi mwilini
Fahamu Moja ya dalili kuu za nyongo kuzidi mwilini ni pamoja na;maumivu ya tumbo upande wa kulia chini ya mbavu. Maumivu haya mara nyingi hutokea wakati kibofu cha nyongo kinapojaa au kutanuka kwa sababu ya mawe ya nyongo au mkusanyiko wa nyongo kwenye kibofu cha nyongo. Maumivu haya yanaweza kuwa ya kudumu au yanayojitokeza mara kwa mara.
Dalili za nyongo kuzidi mwilini zinaweza kujumuisha;
- maumivu ya tumbo upande wa kulia chini ya mbavu,
- kichefuchefu,
- kutapika,
- kuwa na rangi ya njano kwenye macho na ngozi (jaundice),
- kuhisi kujaa au kuvimba kwa tumbo,
- Pamoja na mabadiliko katika rangi ya mkojo au kinyesi.
Ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam haraka ikiwa unaona dalili hizi, au kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane ndani ya @afyaclass.
Soma Zaidi hapa chini,Dalili za nyongo kuzidi mwilini;
-Kichefuchefu na kutapika ni dalili nyingine za nyongo kuzidi mwilini.
Mkusanyiko wa nyongo mwilini unaweza kusababisha hali ya kuhisi kichefuchefu na kutapika. Hali hii inaweza kuzidi hasa baada ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo vinahitaji nyongo nyingi kusagwa.
Unaweza Kutapika matapishi ya rangi ya kijani na njano(greenish-yellow fluid (bile).
– Jaundice au kuwa na rangi ya njano kwenye macho na ngozi ni ishara nyingine inayoweza kutokea wakati nyongo inapozidi mwilini.
Hii hutokea wakati nyongo(bile),inapoingia katika damu na kusambazwa mwilini. Kuwa na rangi ya njano kwenye macho na ngozi inaweza kuwa dalili ya shida katika ini au kibofu cha nyongo.
– Kuhisi kujaa au kuvimba kwa tumbo ni dalili nyingine inayoweza kutokea wakati nyongo inapozidi mwilini.
Hii inaweza kusababishwa na uvimbe wa kibofu cha nyongo au mfumo wa mkojo. Wakati mwingine, uvimbe huu unaweza kusababisha maumivu na kufanya tumbo kuonekana kubwa.
– Mabadiliko katika rangi ya mkojo au kinyesi ni dalili zingine ambazo zinaweza kuashiria nyongo kuzidi mwilini.
Mkojo unaweza kuwa na rangi ya giza,njano au rangi ya machungwa kutokana na uwepo wa nyongo, pia Kinyesi kinaweza kuwa na rangi iliyokolea zaidi tofauti na rangi yake ya kawaida.
Wakati mwingine kinyesi kinaweza kuwa na rangi ya kijivu kutokana na ukosefu wa nyongo mwilini.
Ni muhimu kutambua kuwa dalili hizi zinaweza kuwa za jumla na zinaweza kuhusishwa na matatizo mengine ya kiafya. Hivo ni muhimu kupata utambuzi sahihi kutoka kwa daktari au wataalam wa afya ili kufahamu chanzo cha matatizo yako na kupata matibabu sahihi.
Vipimo:
Baada ya kupata dalili hizi unaweza kufanya vipimo vya damu, skana ya ultrasound, au vipimo vingine vya kufahamu afya ya ini na kibofu cha nyongo ili kubaini tatizo na kuanzisha matibabu yanayofaa.
Usisite kutafuta msaada wa matibabu ikiwa unaona dalili za nyongo kuzidi mwilini.
NB: Nyongo ikizidi mwilini unakuwa kwenye hatari ya kupata tatizo lingine linalojulikana kama Bile reflux.
Bile reflux ni tofauti na Acid reflux, Soma Zaidi hapa kuhusu tatizo la Acid reflux
Bile reflux ni nini?
Bile reflux ni tatizo ambalo huhusisha nyongo ambayo huzalishwa na Ini kurudi tumboni na kwa baadhi ya kesi hupanda mpaka kwenye umio(esophagus)
Hizi hapa ni dalili za Bile Reflux
Inaweza kuwa vigumu kutofautisha Bile reflux na gastric acid reflux. Dalili zake zinaweza kufanana na hali hizi zote mbili huweza kutokea kwa Wakati mmoja,
Ingawa, Bile reflux ni tofauti na Acid reflux, Soma Zaidi hapa kuhusu tatizo la Acid reflux
Hizi hapa ni baadhi ya dalili za Bile reflux;
- Kupata Maumivu ya tumbo upande wa juu ambayo yanaweza kuwa makali
- Kupata kiungulia mara kwa mara
- Kuhisi hali ya kichefuchefu
- Kutapika matapishi ya rangi ya kijani na njano(greenish-yellow fluid (bile)
- Mara chache unaweza kupata shida ya kukohoa
- Pamoja na Uzito wa mwili kupungua
Hitimisho:
Usisite kutafuta msaada wa matibabu ikiwa unaona dalili za nyongo kuzidi mwilini pamoja na dalili hizi za tatizo la Bile reflux au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.