Faida na hasara za kukanda mwili
Watu wengi wana Desturi ya kukanda mwili kwa maji ya moto hasa kwa wakina mama baada ya kujifungua,
Je, kukanda mwili maji kiafya ipoje?
Madhara ya kukanda wazazi kwa maji ya moto,bila shaka wanawake wengi au watu wengi kwenye jamii hawajui kama kuna madhara ya kumkanda mama ambaye ndyo katoka kujifungua,kwani ni kitendo ambacho kimezoeleka kwenye jamii nyingi, na wengi wao huamini kama Tiba kwa mama ambaye ametoka kujifungua.
MADHARA YA KUKANDA WAZAZI KWA MAJI YA MOTO NI PAMOJA NA;
– Kumuweka mama baada ya kujifungua kwenye hatari ya kupata maambukizi mbali mbali ya magonjwa
– Kumsababishia mama ambaye kajifungua maumivu makali ya mwili ikiwemo ukeni
– kuzuia mama baada ya kujifungua kupona kwa haraka zaidi
– Kufanya uharibifu wa kwenye maumbile yake au sehemu za siri
– Kusababisha tatizo la kulegea kwa misuli ya ukeni
– Mama baada ya kujifungua kupata majeraha ambayo huweza kutokana na maji ya moto
– Mama kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua, kwani maji moto hufungua mishipa ya damu iliyojifunga mara baada ya mtoto kutoka na pale damu huanza kuvuja upya
– Mama baada ya kujifungua kupata shida ya kufumuka nyuzi alizoshonwa kama aliongezewa njia wakati wa kujifungua
– Uke wa mama baada ya kujifungua kutengeza uwazi,hali ambayo huweza kusababisha matatizo mengine kama vile uke kujaa hewa na kujamba
– Mama baada ya kujifungua kupata shida ya kuwa na malenge lenge ukeni pamoja na kutanuka misuli ya ukeni kwani wengi wao hukalishwa kwenye kigoda wakati wa zoezi hili
– Fahamu mama akijifungua hupoteza maji mengi mwilini hivo maji hupungua sana mwilini na kusababisha mishipa ya damu kusinyaa, endapo mama huyu atakandwa na maji ya moto huzidi kulainisha mishipa ya damu na kufanya itanuke, hali ambayo huweza kusababisha presha ya damu kupungua na kusababisha maradhi ya moyo baada ya kujifungua tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama postpartum carsiomypathy
– Mwili wa mama aliyejifungua kuweza kuvimba, baadhi ya wakina mama wanaokandwa na maji moto baada ya kujifungua hupatwa na tatizo lingine la mwili kuvimba n.k
– Kusababisha vifo kwa wakina mama baada ya kujifungua, soma hapa chini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitoa ufafanuzi kuhusu swala hili la kuwakanda na maji ya moto wanawake wakishajifungua, mnamo Mwaka 2019 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama nakusema ni hatari zaidi kwao.
Wizara ilisema kwamba kukandwa na maji ya moto kunaweza kusababisha mama kutokwa na damu nyingi na hata kifo.
“Hatuwezi kushauri wanawake waliojifungua kukandwa maji ya moto, japo suala hilo limezoeleka kwa wengi, lakini hakuna uthibitisho wa kitaalamu wa kumponya mwanamke kwa kutumia maji hayo isipokuwa kumletea madhara,” Maelekezo ya Wizara
Mbali na wanajamii wenyewe pia wakunga wa jadi wengi huendelea kuamini kwamba kumkanda na maji moto mama aliyejifungua ni muhimu sana kwani husaidia kuondoa uchafu uliosalia tumboni baada ya mtoto kutoka,je hii ni kweli?
Hiyo ni dhana tu na hakuna ukweli wowote juu ya hili pia ifahamike kwamba, hakuna uchafu wowote unaotakiwa kutolewa na maji ya moto au kwa kukandwa kwani uchafu wote ikiwemo placenta au kondo la nyuma hutolewa na wataalam wa afya wakati mama anajifungua na hata mabaki yote ikiwemo mabonge ya damu hutolewa yote nje kwani yakibaki huweza kusababisha tatizo la mama kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua,hivo ifahamike kwamba mama anasafishwa vizuri hakuna kitu chochote kinabakishwa ndani baada ya kujifungua,
Swala la kukandwa na maji moto,kuminywa au eti kurudisha uke kwenye hali yake ya kawaida kwa mama baada ya kujifungua halina mantiki yoyote na badala yake kwa kufanya hivo unaendelea kuharibu uke au maumbile ya mwanamke na kusababisha madhara mengine.
Hata hivyo, dhana hiyo ilijengeka zaidi na kupata mashiko zamani kwa kile walichodai kwamba kulikuwa hakuna hospital za kutosha au ambazo zipo karibu na maeneo ya watu walio wengi,hivo watu kwenye jamii walikuwa wanaamini hiyo ni miongoni mwa tiba kwa mama ambaye kajifungua na yupo nyumbani.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.