Fibroids ni ugonjwa gani
Fibroids, ambapo pia huitwa myoma, ni uvimbe usio wa saratani (benign) unaokua katika au kwenye kuta za kizazi (uterus) cha mwanamke,
Hivo basi, Fibroids ni uvimbe unaoweza kutokea kwenye Kizazi lakini sio Saratani.
Uvimbe huu unaweza kuwa wa ukubwa tofauti, kutoka kwa udogo usioonekana kwa macho hadi kwa ukubwa unaoweza kusababisha kizazi kubadilika umbo na ukubwa.
Chanzo cha Fibroids
Chanzo halisi cha fibroids hakijulikani, lakini kuna visababishi kadhaa vinavyohusishwa na ukuaji wa fibroids, ikiwa ni pamoja na:
– Mabadiliko ya homoni:
Homoni za estrogen na progesterone, zinazochochea ukuta wa kizazi kukua kila mwezi kama sehemu ya mzunguko wa hedhi, pia zinaaminika kuchochea ukuaji wa fibroids.
– Sababu za kijenetiki:
Fibroids inaweza kurithiwa katika familia.
– Sababu zingine:
Kama vile uzito wa mwili ulio juu(kuwa na uzito mkubwa/overweight), upungufu wa vitamini D, na matumizi ya pombe, pia yamehusishwa na ukuaji wa fibroids.
Dalili za Fibroids
Baadhi ya wanawake wenye fibroids hawapati dalili zozote, huku wengine wakikumbwa na dalili zifuatazo:
- Kupata Menstruation au damu ya hedhi nzito au kwa muda mrefu zaidi ya kawaida
- Kupata Maumivu,shinikizo au hali ya mkazo katika pelvis
- Kupata Maumivu wakati wa kujamiiana
- Kukojoa Mara kwa mara au kupata hisia za haraka za kukojoa
- Kupata choo kigumu au kukosa choo Constipation
- Kupata Maumivu ya miguu
- au kupata maumivu chini ya mgongo n.k
Hakikisha unawahi hospital ikiwa unapata dalili hizi;(See your doctor if you have:)
1. Maumivu ya Pelvic hayaishi licha ya kutumia dawa za kuyatuliza
2. Unapata damu ya Hedhi nzito au maumivu makali ambayo hukusababisha hata ushindwe kufanya chochote
3. Unapata damu vitone vitone kila mara au unapata hedhi katikati ya mwezi
4. Ukikojoa mkojo haushi
5. Unapata uchovu ambao hauishi, na mwili kuwa dhaifu au kukosa nguvu kabsa,
dalili hizi huweza kuashiria pia tatizo lingine la Upungufu wa damu(anemia) ambalo unaweza kuwa nalo kutokana na kuvuja damu nyingi na kwa muda mrefu.
Madhara ya Fibroids(Complications)
Mara nyingi Tatizo la Uterine fibroids sio hatari sana kwa afya yako. Ingawa huweza kuleta maumivu na kusababisha madhara zaidi hasa usipopata matibabu.
Moja ya madhara ni kusababisha shida ya kushuka kwa seli nyekundu za damu(Red blood cells-RBCs) au kusababisha tatizo la Upungufu wa damu(anemia)
Hali hiyo inaweza kusababisha uchovu kutokana na kupoteza damu nyingi. Ikiwa unavuja damu nyingi wakati wa kipindi chako cha Hedhi, daktari wako anaweza kukuambia kuhusu kupata zaidi madini chuma(iron supplement) ili kuzuia au kusaidia kudhibiti upungufu wa damu mwilini. Wakati mwingine, mtu mwenye upungufu wa damu anahitaji kupewa damu kutoka kwa watu wengine(Blood transfusion), kutokana na kupoteza damu nyingi.
Utambuzi wa Fibroids
Fibroids mara nyingi hugundulika wakati wa uchunguzi wa kawaida wa pelvic. Vipimo vya ziada kama ultrasound ya pelvic, MRI, na aina nyingine za uchunguzi zinaweza kufanywa kuthibitisha uwepo na ukubwa wa fibroids.
Matibabu ya Fibroids
Matibabu ya fibroids hutegemea ukubwa wa fibroids, dalili, umri, afya ya jumla ya mwanamke, na kama anataka kuzaa siku za usoni.n.k
Matibabu yanaweza kujumuisha:
✓ Udhibiti wa dalili: Dawa za kutuliza maumivu na dawa za homoni kudhibiti dalili zingine huweza kutumika
✓ Njia za upasuaji: Kama vile myomectomy kwa kuondoa fibroids, au hysterectomy kwa kuondoa kizazi kizima (chaguo la mwisho, hasa kwa wanawake ambao hawataki kuzaa tena).
✓ Tiba zisizo za upasuaji: Kama vile utaratibu wa embolization ya artery ndani ya kizazi au uterine, ambayo inapunguza damu inayotiririka kwenye fibroid, na kusababisha ipungue ukubwa.n.k
Kwa wanawake wengi, fibroids si hatari na zinaweza kudhibitiwa na matibabu yanayolenga kupunguza dalili.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.