TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba kuanzia mchana wa leo Aprili 16, 2024.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia saa 9:30 mchana wa leo Jumanne Aprili 16, 2024.
TMA imetoa tahadhari ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya
Hindi.
Maeneo hayo ni ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mamlaka hiyo imesema uwezekano wa kutokea kwa hali hiyo ni mkubwa na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.
TMA pia imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mamlaka hiyo imesema uwezekano wa kutokea ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.
Athari zinazoweza kujitokeza kwa mujibu wa TMA ni mafuriko, kuathirika kwa baadhi ya maeneo na shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini, ikiwataka wahusika kuchukua hatua.
Aprili 17, 2024
Mamlaka imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.
Pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
TMA imesema uwezekano wa kutokea ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea pia ni wastani.
Athari hizo kwa mujibu wa TMA ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi
na usafirishaji baharini.
Aprili 18, 2024
TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na Lindi pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Pia angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Imesema uwezekano wa hali hiyo kutokea ni wastani na kiwango cha athari pia ni cha wastani.
Mamlaka imetoa taarifa hiyo ikitaka kuzingatiwa na wahusika kujiandaa, kwani athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.
Aprili 19, 2024
TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na Lindi pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mbali na hayo, imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa ya TMA imesema uwezekano wa kutokea hali hiyo ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea pia ni wastani.
Athari hizo kwa mujibu wa TMA ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini. Ikitaka angalizo hilo kuzingatiwa.
Aprili 20, 2024
TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya Mkoa wa Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.
Pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mamlaka imesema uwezekano wa hali hiyo kutokea ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.
TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.