MATIBABU YA ULOTO YA BMH YAZUNGUMZIWA BARAZA LA MAWAZIRI EAC
Akifungua Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Afya EAC, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) Waziri wa Afya, amesema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili maendeleo ya Sekta ya Afya katika Jumuiya na kuboresha maeneo mbalimbali ya sekta hiyo.
“Pamoja na agenda nyingine Tanzania itawasilisha agenda ya uanzishwaji wa Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto kwa watoto wenye selimundu (Sickle Cell), kwa kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imeshaanza kutoa huduma ya upandikizaji uloto na watoto kumi wameshapatiwa matibabu na wamepona kabisa na huduma ya matibabu haya yanaendelea, hivyo tunaona umuhimu wa kuanzisha Kituo cha Umahiri kupitia Hospitali ya Benjamin Mkapa,” alisema Ummy.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaendelea kukuwa kwa kasi kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo, hivyo Mkutano huo utatazama mikakati mbalimbali ya kuhakikisha ya kudhibiti magonjwa hayo kwa nchi wanachama wa EAC.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy, “Tanzania imeshaanza kufanyia kazi kwa kuanzisha hamasa ya mazoezi na kesho Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atazindua mazoezi maalumu yatakayo kuwa yanafanyika kila siku ya jumamosi.
“Wataalamu wanatuambia njia moja wapo ya kudhibiti magonjwa ysiyo ya kuambukiza ni kufanya mazoezi,” alisema Ummy.
Kwa upande wake, Mary Mothoni, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Kenya, ameeleza umuhimu wa kuelimisha jamii za EAC kuwa afya inaanzia nyumbani.
“Kama jamii zetu zitaelewa afya inaanzia nyumbani zitaandaa mazingira yote mazuri ya kuhakikisha wanakuwa salama na afya nzuri,” alisema.
Aliongeza kuwa ukiacha mazingira ya nyumbani kwako yana mazalia ya mbu familia itapata Malaria, akiongeza kuwa kama familia haitoandaa maji safi na salama shida itapatikana kwenye familia hivyo afya inaanzia nyumbani. @wizara_afyatz @ummymwalimu @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano
Benjamin yaendelea kupandikiza betri kwenye moyo.
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma upasuaji wa kupandikiza betri kwenye moyo kwa watu watatu leo.
Upandikizaji wa betri kwenye moyo ambao kitaalamu inaitwa _pacemakers_ _implantation_ unafanyika kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa kwa mtu wa kawaida ambayo ni 60-100 kwa dakika.Wengi wao huwa ni chini ya 40.
Mkuu wa Kliniki ya Moyo wa BMH, Daktari Bingwa wa Moyo, Happiness Kusima, amesema leo kuwa BMH imefikisha upandikizaji kwa watu 18 toka huduma ianzishwe mwaka 2021.
“Jana tumepandika watu watatu (3), leo tutapandikiza watu wawili,” amesema Daktari huyo Bingwa wa Moyo.
Dkt Happiness amesema upandikizaji huu unafanyika kwenye kambi ya pamoja kati ya Madaktari Bingwa wa Moyo wa BMH na Daktari Bingwa wa Moyo, George Longopa, kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
Kambi hii ya moyo ya pamoja kati ya BMH na JKCI imeanza leo na itakamilika kesho. @wizara_afyatz @ummymwalimu
Benjamin yafanya matibabu ya moyo kwa kutumia mshipa wa mkono kwa mara ya kwanza.
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanya uchunguzi wa moyo kwa mgonjwa kwa kutumia mshipa wa mkono kwa mara ya kwanza.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha maabara maalum ya uchunguzi wa Moyo(Catheterization Laboratory -CathLab) cha Hospitali hio, Dkt Kelvin Masava, uchunguzi na matibabu kwa njia hio mbali na kuwa na faida nyinginezo lakini inampunguzia mgonjwa muda wa kukaa hospitalini.
“Mgonjwa anarejea kwenye shughuli zake kwa wepesi na haraka ikilinganishwa na njia ya kupitia kwenye mshipa wa mguuni tuliyokuwa tukitumia wakiitumiaa awali,” anasema
Anafafanua kuwa utaratibu huu unamuwezesha mgonjwa kunyanyuka na kutembea mwenyewe mara tu baada ya kupata huduma tofauti na apo awali.
“Njia ya mshipa wa mguuni ilihitaji mgonjwa kukaa si chini ya saa sita baada ya huduma pasipo kuinuka kitandani au kukunja mguu tofauti na hii ambapo anainuka kutembea mwenyewe na baada ya saa chache anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyo hiyo,” ameongeza. @wizara_afyatz
Tumeokoa maisha ya watu wengi waliopatwa na tatizo la kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest)-Benjamin Mkapa.
IDARA YA MAGONJWA YA DHARURA YA BMH YATIMIZA MIAKA MITANO
Idara ya Magonjwa ya Dharura (EMD) ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imetimiza miaka mitano ya huduma leo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa BMH,Dkt George Dilunga, amesema Idara hiyo imekuwa ikikuwa na kuongezeka katika utoaji huduma mwaka hadi mwaka. Idadi ya wateja wanaohudumiwa na Idara ya Magonjwa ya Dharura imeongezeka kutoka wateja 1000 kwa mwezi miaka mitano iliyopita mpaka 3500 kwa sasa.
“Tumeokoa maisha ya watu wengi waliopatwa na tatizo la kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest),” amesema.
Amesema EMD itaendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwemo uokozi katika majanga kama ajali na mafuriko yanayotokeaa sehem mbalimbali nchini.
“EMD ya BMH ilikuwa ni miongoni mwa watoa huduma waliowahi kwenda kutoa huduma Manyara kulipotokea maporoko ya tope yaliyosababishwa na mvua kubwa mwaka jana,” amesema Dkt Dilunga.
Aidha amebainisha kuwa kuna mipango endelevu ya kuhakikisha kuwa huduma bora na za wakati zinaendelea kutolewa idarani hapo ikiwemo kuhakikisha wagonjwa hawakawii kupata huduma za dharura.
Vilevile amebainisha kuwa mipango mingine endlevu ipo kuhakikisha wataalamu zaidi wa magonjwa ya dharura wanapatikana na kupewa mafunzo ili kuendelea kutoa huduma zilizo bora.
“Tuna mpango pia wa kuendeleza huduma za ambulance (EMS) pamoja na kuweka mfumo mzuri wa uokozi wagonjwa wanaopata dharura za kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest) wawapo hospitalini ujulikanao kama Code Blue” alimalizia Dkt. Dilunga. @wizara_afyatz