Habari njema hii. Lakini nisisitize kuwa UKIMWI bado upo na kila mmoja wetu anapaswa kuchukua Hatua.
—
Utafiti wa Hali ya UKIMWI nchini (Tanzania HIV Impact Survey – THIS 2022/23) umeonyesha kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) kuwa kimepungua kutoka asilimia 4.9 mwaka 2016/17 hadi asilimia 4.4 mwaka 2022/23.
Mikoa mitatu yenye kiwango cha juu cha maambukizi katika Utafiti huu ni Njombe (12.7%), Iringa (11.1%) na Mbeya (9.6%), na.
Mikoa yenye maambukizi ya chini ni Kigoma (1.7%), Manyara (1.8%) na Lindi (2.6%).
Kwa Utafiti wa mwaka 2016/17, mikoa iliyoongoza kwa kiwango kikubwa kwa maambukizi ilikuwa ni Njombe (11.4%), Iringa (11.1%) na Mbeya (9.3%). Mikoa iliyokuwa na maambukizi ya chini ilikuwa ni Kigoma (2.9%), Manyara (2.3% na Lindi (0.3%).
Katika kufikia malengo ya 95-95-95 ifikapo Mwaka 2025, Kiwango cha watu wanaofahamu hali yao ya maambukizi kuhusu VVU ni asilimia 82.7 kwa 2022/23 kulinganisha na asilimia 60.6 kwa mwaka 2016/17,
Kiwango cha Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) na wanatumia dawa za Kufubaza VVU (ARV) ni asilimia 97.9 kulinganisha na asilimia 93.6 mwaka 2016/17
Aidha, kiwango cha wanaotumia dawa na wamefubaza VVU ni asilimia 94.3 mwaka 2022/23 kulinganisha na asilimia 87 mwaka 2016/17.
Nitumie fursa hii kumshukuru kwa dhati Rais wetu Dkt @SuluhuSamia kwa kutuwezesha kufikia mafanikio haya ikiwemo kuhakisha huduma bora za tiba na matunzo kwa WAVIU. Aidha nimamshukuru Mhe Waziri Mkuu @KassimMajaliwa_ kwa kutuongoza vyema katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Nawashukuru Viongozi na Wataalam wote wa sekta ya afya nchini mwa kujitoa kwao ktk mapambano dhidi ya UKIMWI ikiwemo kuwahudumia WAVIU. Ninayashukuru mashirika ya kiraia kwa kazi nzuri. Kipekee ninawashukuru Wadau wetu hususani @GlobalFund @PEPFAR @USAIDTanzania @UNAIDS kwa kuchangia rasilimali fedha na utaalamu katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Asanteni sana Wananchi kwa kushiriki vita hii. Ninaomba tuendee kuchukua hatua ili kujikinga na VVU na endapo tayari una maambukizi basi usiache kutumia Dawa za ARVs. Kwa Pamoja tunaweza kutokomeza UKIMWI nchini Tanzania #MtuNiAfya