Madhara ya damu kuwa nyingi mwilini
Moja ya vitu vya kuangalia wakati unapima wingi wa damu ni pamoja na kiwango cha Hemoglobin, Wakati seli nyekundu za Damu(Red blood cells) zinapokuwa na kiwango kikubwa cha hemoglobin (Hgb) tunapata majibu kwamba damu yako ni nyingi.
#Soma Zaidi kuhusu Vitu vyote vinavyotengeneza damu
Hemoglobin ni proteins ambazo husababisha seli nyekundu za damu kuwa na rangi yake nyekundu. Zinasaidia pia kwenye kubeba oxygen kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye sehemu zingine za mwili,
Pia hewa ya carbon dioxide (CO2) kutoka kwenye sehemu za mwili wako kurudi kwenye mapafu. jina lingine la hemoglobin hizi kuwa nyingi hujulikana kama polycythemia.
Je, ni kiwango kipi cha hemoglobin kuwa juu?
Uli tuseme una damu nyingi maana yake hemoglobin ni nyingi, sasa je, ni kipi kiwango cha hemoglobin tukikiona tunasema damu yako ni nyingi?
Fahamu hapa baadhi ya Viwango hivo;
- Zaidi ya 16.5 grams per deciliter (g/dL) kwa mtu mzima jinsia ya kiume
- Zaidi ya 16 g/dL kwa mtu mzima jinsia ya kike
- Zaidi ya 16.6 g/dL kwa mtoto ambaye ni child.
- Zaidi ya 18 g/dL kwa mtoto ambaye ni infant.
Madhara ya damu kuwa nyingi mwilini
Kama damu yako imezidi mwilini unaweza kukutana na changamoto kama hizi;
1. Kupata shida ya Kizunguzungu mara kwa mara
2. Ngozi kuchubuka kwa urahisi au damu kutoka nyingi kwa kajeraha kadogo tu(Easy bruising or bleeding).
3. Kutokwa na jasho kupita kiasi,hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama hyperhidrosis.
4. Mwili kuchoka sana,Fatigue
5. Kupata maumivu makali ya kichwa mara kwa mara.
6. Joint kuvimba kwa baadhi ya Watu
7. Uzito wa mwili kupungua bila sababu ya msingi
8. Macho au ngozi kuwa manjano au tunasema tatizo la adult jaundice.
#Chanzo cha Damu kuwa Nyingi,Soma Zaidi hapa kufahamu
Vitu hivi huweza kuchangia kiwango cha hemoglobin kuwa juu;
– Magonjwa mbali mbali kama vile;
- Chronic obstructive pulmonary disease (COPD).
- Magonjwa ya moyo kama vile Congenital heart disease.
- Tatizo la Emphysema.
- Saratani ya kibofu(Kidney cancer).
- Saratani ya Ini(Liver cancer).
- Tatizo la Polycythemia vera.
- Tatizo la Pulmonary fibrosis.
– Sababu Zingine za kiwango cha hemoglobin kupanda sana ni pamoja na:
(1) Kuwa kwenye mazingira yenye Carbon monoxide.
(2) Upungufu wa maji mwilini(Dehydration).
(3) Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile dawa jamii ya anabolic steroids au erythropoietin-stimulating agents.
(4) Kubadilisha mazingira na kwenda nyanda Za juu yaani high altitude.
(5) Uvutaji wa Sigara n.k.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.