Madhara ya nyama nyekundu
Nyama nyekundu maarufu kama “Red Meat” ni nyama ambayo wataalam wengi wa afya wamekuwa wakiizungumzia hasa kwa upande wa kuleta madhara kwenye afya zetu japo sio kama ina hasara tu bali hata faida zipo(kila kitu chenye faida kina hasara zake pia).
Tafiti mbali mbali za afya hufanyika kila siku kuhusiana na madhara ya nyama nyekundu yaani Red Meat kwenye afya ya Mwili wa Binadamu, na katika makala hii tumechambua baadhi ya madhara katika tafiti mbali mbali za afya kuhusu madhara ya nyama nyekundu,
MADHARA YA KULA NYAMA NYEKUNDU NI PAMOJA NA;
– Nyama nyekundu(Red Meat) huchangia mtu kupatwa na magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwa ni pamoja na tatizo la mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba,
hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta yaani SATURATED FAT na matokeo yake ni kuwa na kiwango kikubwa cha Cholestrol(Lehemu) mwilini, Cholestrol nyingi mwilini ni mojawapo ya vihatarishi vikubwa vya magonjwa mbali mbali ikiwemo magonjwa ya moyo
– Nyama nyekundu(Red Meat) huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo la saratani au Kansa ya Tumbo,
– Pia kuna utafiti ambao umefanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa nchini Marekani, umebaini kwamba asilimia kubwa ya watu wanaopenda kula nyama nyekundu yaani Red Meat kwa kiasi kikubwa kwenye maisha yao, hufariki mapema zaidi kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.
JE NYAMA YA NGURUWE NI NYAMA NYEKUNDU?
Swali hili watu wengi wameniuliza sana, kwani nyama ya Nguruwe ukiiangalia sio nyekundu ni nyeupe, je nayo ipo kwenye kundi la nyama nyekundu?
Ukweli ni kwamba hata nyama ya nguruwe ipo kwenye kundi la Nyama nyekundu hata kama kwa muonekano wa nje ni nyeupe, soma hii hapa,
Kutokana na utafiti wa Wizara ya Kilimo ya nchini Marekani, kiwango cha protini aina ya ‘myoglobin’ kilichomo kwenye misuli ya nyama yoyote ndicho kinachoonesha aina ya nyama,
Hivo basi,Nyama ya nguruwe inawekwa kwenye kundi la nyama nyekundu yaani Red Meat kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha protein aina ya ‘myoglobin’ kuliko kile kilichomo kwenye nyama nyeupe za kuku na samaki.
Hivo unashauriwa kupunguza sana ulaji wa nyama nyekundu yaani Red Meat,kwa sababu matumizi ya kiwango kikubwa cha nyama nyekundu sio salama kwa afya yako.
Lakini pia mbali na ulaji wa nyama nyekundu,wataalam wa afya hushauri kuepuka kula nyama zenye mafuta mengi,kwani mafuta haya huweza kuwa chanzo cha magonjwa mbali mbali mwilini kama vile magonjwa ya moyo n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.