Madhara ya vumbi la kongo
Soma hapa kufahamu madhara ya kutumia Vumbi la Kongo kwa afya yako,
- Je Vumbi la Kongo ni nini?
- Je madhara ya vumbi la Kongo ni yapi?
- Kwanini Wanaume wanatumia Vumbi la Kongo?
Maswali yote haya utapata Majibu hapa,kwenye makala hii, Soma zaidi hapa chini
MADHARA YA KUTUMIA VUMBI LA KONGO
Vumbi la kongo ni jina ambalo ni maarufu sana na linatumika kwa dawa ambayo hutumiwa sana na wanaume kwa lengo la kuwaridhisha wapenzi wao au wake zao.
Dawa hii ya vumbi la kongo hupakwa kwenye uume nusu saa kabla ya Mwanaume kushiriki tendo la Ndoa ili ifanye kazi vizuri,
Kinachotokea ni kwamba, ndani ya dawa hii kuna kemikali ambazo zimeweka kwa lengo la kutia ganzi uume hivo kumfanya mwanaume ashiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu zaidi.
MADHARA YA KUTUMIA VUMBI LA KONGO
Madhara ya kutumia vumbi la kongo kwa wanaume ni pamoja na;
– Mwanaume kushindwa kushiriki tendo la ndoa kama hajatumia dawa hii ya vumbi la kongo
– Kuathiri mishipa ya uume na kusababisha uume wa mwanaume kushindwa kusimama moja kwa moja kutokana na athari za kutiwa ganzi, hivo ikabaki kazi moja tu ya kukoja na sio kufanya mapenzi
– Uume kusinyaa kabsa na kulegea hata wakati wa kushiriki tendo la ndoa
– Kukosa hamu ya kufanya mapenzi na kufurahia tendo
– Pia matumizi ya dawa kama hizi za kupaka kwenye uume huweza kusababisha fangasi wa sehemu za siri kwa mwanamke endapo mmeshiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga au Condom
– Mwanaume kupoteza kabsa uwezo wa kurudia tendo la Ndoa mara ya pili
Epuka matumizi ya vitu hivi ni hatari kwa afya yako, kama una tatizo la kukosa nguvu za kiume kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya matibabu sahihi
#SOMA pia Zaidi hapa; Kuhusu matumizi ya vumbi la kongo na madhara yake.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.