Chanzo cha tatizo la Maumivu ya Makalio na Tiba yake
Unaweza usifikiri chochote kuhusu makalio yako wala hata usiyaangalie ila ukianza kupata maumivu lazima utaanza kufwatilia nini chanzo chake,
Makalio kwa kiasi kikubwa yametengenezwa na misuli ambayo ni fat and gluteal muscle, misuli hii huweza kupatwa na Majeraha au maambukizi ya magonjwa ambayo huweza kupelekea maumivu makali ya makalio.
Kulingana na chanzo chake,Maumivu hayo huweza kuwa makali sana kisha kuambatana na matatizo mengine kama vile;
- Kupata shida ya kutembea au miguu kuwa dhaifu sana,kufa ganzi n.k
- Kushindwa kujizuia haja kubwa au haja ndogo
- Kuwa na Vidonda kwenye makalio ambayo haviponi
- Kuwa na Homa au joto la mwili kuwa juu sana mfano;104°F (40°C) au Zaidi
- Maumivu ambayo hutokea pale tu unataka kutembea,na kukusababishia kushindwa kutembea n.k
HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU ZA TATIZO LA MAUMIVU MAKALI YA MAKALIO
1. Kuchubuka(Bruising), Miongoni mwa sababu kubwa ambayo husababisha maumivu ya makalio kwa watu ni pale wanapopata michubuko kutokana na sababu mbali mbali kama vile kupata ajali,kuanguka n.k
Sehemu ya michubuko hubadilika rangi kutokana na damu kuvuja kutoka kwenye vimishipa vilivyoharibiwa kwenye ngozi ya eneo la makalio lililopata michubuko.
Michubuko huweza kupelekea maumivu ya makalio ambayo huanzia eneo lenye michubuko kisha kusambaa maeneo mengine.
2. Tatizo la Misuli kukaza yaani Muscle strain, Mtu huweza kupata maumivu ya makalio kama moja ya misuli hii imepata shida ya kukaza;
- gluteus maximus,
- gluteus medius
- Au gluteus minimus.
Na hapa asilimia kubwa chanzo cha misuli hii kukaza na kusababisha maumivu ya makalio kwa watu ni kutokana na kufanya mazoezi kupita kiasi, kutokufanya warming up kabla ya kuanza mazoezi,kuondoka kwa gafla au kusimama kwa gafla n.k
3. Tatizo kwenye sciatic nerve, ambalo hupelekea mtu kuhisi kuungua kuanzia kwenye Sciatic nerve na kupata maumivu makali ya makalio yanayoanzia sehemu ya chini ya mgongo(lower back),kupita kwenye makalio kwenda mpaka miguuni
4. Tatizo la Bursitis ambalo huhusisha kuwa na vijifuko ambavyo maji maji yamejikusanya(fluid-filled sacs) hasa hutokea kwenye maeneo ya mabega,hips,magoti na kwenye kiwiko
Lakini pia huweza kutokea sehemu ya makalio ambapo kwa kitaalam hujulikana kama ischial bursa, Hii hupelekea maumivu ya makalio hasa wakati unataka kukaaa au Kulala,
maumivu haya huweza kwenda na kusambaa mpaka kwenye mapaja yako.
5. Tatizo la Herniated disk, ambalo huweza kusababisha mgandamizo wa Nerves,Maumivu makali,ganzi n.k
6. Lakini pia kupata tatizo la Degenerative disk disease ambapo mara nyingi umri unavyokuwa mkubwa pingili za mgongoni huweza kulika taratibu,kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi kama zamani, na kisha kupelekea maumivu ya makalio na mapaja.
7. Tatizo la Piriformis syndrome pamoja na Pilonidal cyst
8. Tatizo la Majipu(Perirectal abscess), Unaweza kupata jipu au majipu karibu kabsa na tundu la haja kubwa, hali ambayo huweza kusababisha maumivu makali ya Makalio.
Hivo majipu sehemu ya makalio huweza kuwa chanzo cha maumivu makali ya makalio
9. Lakini pia unaweza kuwa na tatizo la Fistula ambayo huhusisha Sehemu ya haja kubwa(Anus), Hii pia huweza kupelekea maumivu makali ya makalio, hasa pale ambapo utapata maambukizi ya Bacteria kwenye tundu linalotokana na Fistula.
10. Tatizo la Sacroiliac joint dysfunction huweza kusababisha maumivu kuanzia chini ya mgongo,kupita makalioni kwenda Miguuni,
na maumivu yake huwa makali zaidi wakati wa kutembea,kukimbia,au kupanda ngazi
11. Tatizo la Arthritis ambalo huweza kusababisha maumivu ya joints, na tatizo hili likihusisha Hip Joint huweza kusababisha maumivu kwenye makalio pia.
12. Magonjwa kwenye mishipa ya damu(Vascular disease), tatizo kama atherosclerosis huweza kupelekea mishipa ya damu kuziba na kusababisha maumivu ya makalio,
Hii hutokea pale ambapo mishipa iliyoziba ni iliac arteries(mishipa miwili iliyogawanyika kutoka kwenye Aorta) ambayo hugawanyika zaidi na kupeleka damu mpaka miguuni.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.