Msamaria mwema aingia kwenye matatizo baada ya kumkimbiza mfanya Usafi aliyezimia hospitalini.
NIGERIA; Msamaria mwema alia baada ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kumkimbiza mfanya Usafi aliyezimia hospitalini,
Msamaria Mwema huyo amepiga kelele baada ya kukamatwa na kushtakiwa kortini kwa kumpeleka hospitalini mfanyakazi wa Usafi aliyezirai.
Kulingana na mtumiaji mmoja wa mtandao wa X, hamjui mfanya Usafi huyo ambaye alizirai lakini alihisi kuwa ni wajibu wake kama mhudumu wa afya kumpeleka mwanamke huyo hospitalini.
Hata hivyo, baada ya kufika hospitalini, alitakiwa kufungua file na kutoa maelezo kwa ajili ya mfanya usafi huyo lakini baada ya kusema hamfahamu na kushindwa kutoa maelezo yake, mkurugenzi wa hospitali hiyo anadaiwa kumtuhumu kwa kumpiga mfanya usafi huyo na kusababisha polisi kumkamata.
Mtumiaji huyo wa Twitter aliendelea kufichua kuwa yeye na baadhi ya wanafamilia wake sasa wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kushambulia ingawa mfanya Usafi huyo sasa ana fahamu na amepinga madai hayo.