Omeprazole inatibu ugonjwa gani
Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi wa @afyaclass, Leo tumeamua kuichambua dawa hii kazi zake kwa faida ya wengi.
Dawa ya Omeprazole:
Omeprazole ni dawa inayotumika kutibu hali kadhaa ambazo huhusiana na Ongezeko la kiwango kikubwa cha Acid tumboni.
Dawa hii huweza kutumika kutibu matatizo kama vile;
- vidonda vya tumbo( gastric and duodenal ulcers),
- Tatizo la erosive esophagitis,
- Pamoja na gastroesophageal reflux disease (GERD).
GERD; ni tatizo linalohusu acid kurudi kutoka tumboni kwenda kwenye umio au esophagus(acid reflux).
#Soma Zaidi hapa; Tatizo la gastroesophageal reflux disease (GERD).
Pia wakati mwingine omeprazole hutumika ikiwa pamoja na dawa zingine jamii ya antibiotics (mfano, amoxicillin, clarithromycin) kutibu vidonda vya tumbo vinavyotokana na maambukizi ya bacteria aina ya H. pylori bacteria.”
Omeprazole huweza kutumika kutibu tatizo la Zollinger-Ellison syndrome, hali ambayo Tumbo huzalisha kiwango kikubwa sana cha acid.
Pia Omeprazole ni nzuri kwa matibabu ya shida ya dyspepsia, hali inayosababisha tumbo kuwa chungu, kupata kiungulia mara kwa mara, au chakula kutosagwa vizuri.
Usichokifahamu kuhusu dawa ya omeprazole, ni kwamba dawa hii huweza kutumika kuzuia tatizo la kuvuja damu yaani upper gastrointestinal tract bleeding kwa wagonjwa wenye hali mbaya sana.
Ijue Dawa ya Omeprazole:
Omeprazole ni dawa jamii ya proton pump inhibitor (PPI), inafanya kazi kwa kupunguza kiwango cha Acid kinachozalishwa na Tumbo.
Dawa hii inaweza kutolewa kwa cheti cha daktari au bila cheti cha daktari(This medicine is available both over-the-counter (OTC) and with your doctor’s prescription).
Dawa ya Omeprazole inapatikana kwa forms hizi:
- Powder for Suspension
- Tablets
- Capsules
- Au Packet
Haya ndyo Maelezo mafupi kuhusu dawa hii jamii ya Omeprazole….