Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu
Je kuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu?
Zipo dhana mbali mbali na sisi pia kama afyaclass,tumepokea maswali mengi sana,Watu wakiuliza kuhusu Yapi ni Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu?
Katika makala hii tumechambua baadhi ya tips za kukusaidia kujua kuhusu hili;Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu.
Ukweli ni kwamba hakuna kiwango sahihi cha kufanya Mapenzi kwa mtu, hii huweza kutegemea kati ya mtu na mtu, na kutokufanya Mapenzi kwa muda mrefu hakuwezi kuwa na madhara kwa afya yako,
Soma Zaidi hapa Kujua,...
Nanukuu maneno kutoka kwenye Jarida la afya(medicalnewstoday) Wanasema;
"No one should ever feel obliged to have sex. Avoiding sex will not harm a person’s health, and it may even be healthy".
Hakuna Mtu wakunyooshewa kidole au kuhukumiwa kwa kutokufanya Mapenzi kwa muda mrefu, Kuepuka kufanya Mapenzi hakuwezi kuleta madhara kwa afya ya mtu, na badala yake huweza kuwa afya Zaidi kwake.
Ingawa hakuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu, lakini kutokuwa na hisia za Mapenzi kabsa huweza kuwa tatizo la kiafya ambalo huhitaji Matibabu,
Hivo kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa, huweza kutokana na Sababu mbali mbali ambazo zingine ni lazima upate matibabu ya kitaalam.
Nanukuu maneno kutoka kwenye jarida ya afya(Healthline)kuhusu Madhara ya kutokufanya mapenzi muda mrefu
"Despite what you may see on TV, there’s nothing wrong with you if you are not having sex all the time. There is also nothing wrong with you if you never have sex".
Licha ya kile unachoweza kuona kwenye TV au vyanzo vingine vya Taarifa, hakuna ubaya kwako ikiwa hufanyi tendo la ndoa kila wakati. Pia hakuna kitu kibaya kwako ikiwa hujawahi kufanya mapenzi kabsa,
FAQs: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, Kuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu?
Hakuna Mtu wakunyooshewa kidole au kuhukumiwa kwa kutokufanya Mapenzi kwa muda mrefu, Kuepuka kufanya Mapenzi hakuwezi kuleta madhara kwa afya ya mtu, na badala yake huweza kuwa afya Zaidi kwake.
Hitimisho
Hakuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu, na badala yake huweza kuwa faida kwako,
kwani huweza kukupunguzia hatari ya Kupata magonjwa mbali mbali ya Zinaa(Sexual transmitted diseases-STDs)
Ni matumaini yangu kwamba tumejibu vizuri swali lako la;
" Je, Kuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu?".