Wajawazito 43,323 wagundulika kuwa na VVU
Takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha jumla ya Vituo 7,830 sawa na 96% ya Vituo 8,164 vinavyotoa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto viliweza kutoa huduma za kuzuia Maambukizi ya VVU na Kaswende kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto
Jumla ya Wajawazito 1,453,235 sawa na 97.4% ya Wajawazito 1,492,931 waliohudhuria Kliniki walipimwa VVU katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 ikilinganishwa na Wajawazito 1,627,685 sawa na 98.9% ya Wajawazito 1,645,417 waliopimwa katika kipindi kama hicho Mwaka 2022/23
Wajawazito 43,323 sawa na 2.98% ya Wajawazito wote walibainika kuwa na maambukizi ya VVU kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 ikilinganishwa na Wajawazito 47,475 sawa na 2.85% waliobainika kuwa na maambukizi ya VVU kwa kipindi kama hicho Mwaka 2022/23