Rita Na Nida Zaunganishwa Kuwa Taasisi Ya Utambuzi Wa Matukio Muhimu Maishani.
Ofisi ya Mipango na Uwekezaji imetoa tangazo la kuunganishwa kwa Mashirika ya kadhaa yakiwemo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),
na kuunda Taasisi moja inatayohusika na utambuzi wa matukio muhimu maishani.
Lengo la hatua hii ni kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu ya kuwa na Namba moja ya Utambulisho (Single Identification Number).
Mashirika mengine yaliyounganishwa ni Benki ya Kilimo Tanzania na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, Bodi ya Chai na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania, Bodi ya Nyama na Bodi ya Maziwa na Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijjini na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) na SIDO.