Zaidi ya watu bilioni moja duniani wanakabiliwa na unene kupita kiasi.
Zaidi ya watu bilioni moja wanaishi na unene uliokithiri duniani kote, Hizo ni takwimu za makadirio ya kimataifa yaliyochapishwa katika kipindi cha The Lancet.
Hii inajumuisha takriban watu wazima milioni 880 na watoto milioni 159, kulingana na data za mwaka 2022.
Viwango vya juu zaidi viko Tonga na Samoa ya Marekani kwa wanawake na Samoa ya Marekani na Nauru kwa wanaume, na baadhi ya asilimia 70-80% ya watu wazima wanaishi na unene kupita kiasi.
Takwimu za watu wanaokabiliwa na unene Zaidi duniani;
Kati ya nchi 190 hivi, Uingereza inashika nafasi ya 55 kwa wanaume na 87 kwa wanawake.
Wataalamu kimataifa na wanasayansi wanasema kuna haja ya dharura kwenye kufanya mabadiliko makubwa katika jinsi watu wanavyokabaliana na tatizo hili la Unene kupita kiasi(Obesity/fetma).
Unene unaweza kuongeza hatari ya kupata hali nyingi mbaya za kiafya, pamoja na ugonjwa wa moyo, kisukari cha aina ya 2 na saratani kadhaa.
>>Soma hapa Zaidi; Jinsi ya kupunguza Uzito kwa haraka ukiwa nyumbani kwako(Muongozo kamili)