KUUMWA TUMBO BAADA YA TENDO LA NDOA
Shida ya kuumwa tumbo baada ya tendo la ndoa haitokei kwa wanawake tu,inaweza kuwapata wote wanawake na wanaume japo kwa Wanaume hutokea mara chache sana,
na kuna sababu nyingi tu huweza kuchangia tatizo la kuumwa tumbo baada ya tendo la Ndoa kama vile;
1.Kuvutwa na kukaza kwa misuli ya tumbo na kiuno(Abdominal and pelvic Muscle strains) wakati wa tendo la ndoa,
Hali hii hutokea kama vile wakati mtu anafanya mazoezi,na huweza kuchangia mtu kupata maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
2. Hali ya maji ya mwili kupungua(dehydration),misuli kukaza pamoja na misuli kufanya kazi kwenye awkward position huweza kusababisha maumivu ya tumbo ambayo huondoka ndani ya muda mfupi sana.
3. Kufika kileleni, Wakati unafika kileleni misuli ya kiuno au nyonga(pelvic floor) huweza kuvutwa sana bila wewe kupanga yaani Involuntary Muscles contraction,hali ambayo huweza kupelekea maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
4. Tatizo la tumbo kujaa gesi huweza kutokea na kusababisha maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa
5. Tatizo la kupata choo kigumu yaani Constipation huweza kuchangia uwepo wa maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
6. Tatizo la Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo au UTI, na matatizo mengine kama vile interstitial cystitis n.k
7. Magonjwa ya Zinaa(Sexually transmitted infection-STIs), Hasa pangusa (chlamydia) na kisonono(gonorrhea) huweza kusababisha maumivu ya tumbo baada ya tendo la Ndoa.
8. Wakati mwingine maumivu ya kihisia(Emotional trauma) kutokana na mambo yaliyopita au wakati wa tendo huweza kusababisha maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
Hata yali ya hofu na wasiwasi wakati wa tendo huweza kusababisha maumivu ya tumbo baada ya tendo.
KUUMWA TUMBO BAADA YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE
Hizi hapa ni baadhi ya sababu ambazo huweza kuchangia maumivu ya tumbo baada ya tendo la Ndoa kwa Wanawake;
- Uume kuzamishwa zaidi na kwa nguvu sana(Deep penetration), hii huweza kuleta hali ya mkazo au hata michubuko kwenye via vya uzazi vya mwanamke na wakati mwingine maambukizi mpaka kwenye mlango wa uzazi(Cervix).
Kitendo hiki huweza kumsababishia mwanamke maumivu ya tumbo baada ya tendo la Ndoa.
NB:Kumbuka Mapenzi sio vita ni Ujuzi,Usitumie nguvu tumia akili. Wanaume wengi wanafikiri ukifanya mapenzi kwa nguvu sana ndyo unamridhisha mwanamke,
Na mwanamke akilalamika wakati wa tendo haimaanishi anafurahia tendo wengine wanapata maumivu makali sana.
- Tatizo la uvimbe kwenye kizazi(Fibroids) na uvimbe vifuko vya mayai(Ovarian cysts), Tatizo hili pia huweza kuchangia maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
- Kufanya mapenzi kipindi cha Ovulation, baadhi ya Wanawake hupata maumivu ya tumbo endapo wakifanya mapenzi kipindi hiki ambapo yai linatoka kwenye vifuko vya mayai nakuingia kwenye mirija ya uzazi kwa ajili ya urutubishaji.
- Tatizo la Vaginismus,ambapo misuli ya uke hubana yenyewe bila mwanamke kupanga wakati kitu chochote kikiingia ukeni,
Tatizo hili huweza kusababisha maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa kwa baadhi ya Wanawake.
- Maambukizi ya Bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke(Pelvic inflammatory disease-PID)
Tatizo la PID huweza kuchangia maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa kwa baadhi ya Wanawake wenye shida hii.
- Magonjwa ya Zinaa kama vile chlamydia na gonorrhea huweza kuchangia tatizo hili pia.
- Tatizo la Endometriosis pamoja na matatizo mengine kwenye kizazi cha Mwanamke kama vile tatizo la retroverted uterus huweza kuleta maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
KUUMWA TUMBO BAADA YA TENDO LA NDOA KWA WANAUME
Japo ni mara chache sana kwa wanaume kupatwa na tatizo hili la maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa,ila wapo baadhi ya wanaume hupatwa na shida hii, na baadhi ya sababu ni kama vile;
- Uwepo wa tatizo la Prostatitis ambapo huhusisha kuvimba kwa tenzi la kiume yaani Prostate, hali hii huweza kuleta maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.