Vifo zaidi ya watu 400: Ripoti ya Shakahola ilipuuzwa
Tume ya Kitaifa ya haki za Binadamu Kenya – KNHCR, imesema Maafisa wa Serikali na Mamlaka za Polisi Nchini humo walipuuza ripoti za kuaminika ambayo ingeweza kuzuia vifo vya zaidi ya watu 400.
Watu hao, ni wale waliokuwa wakihudhuria mahubiri na mafundisho ya dhehebu lenye utata, katika Kanisa la Mchungaji Paul Mackenzie la Good News International, lililopo Shakahola.
Katika maafa hayo, zaidi ya watu 400 wakiwemo watoto walifariki kutokana na mahubiri yenye kupotosha, wakiamriwa kutokula wala kunywa, huku wengine wakiuliwa na walinzi wa Mackenzie walipotaka kughairi zoezi hilo.