Ugonjwa wa macho unaowapata watu wengi Zaidi Duniani
Katika Makala ya Leo Nimekuelezea baadhi ya magonjwa ya Macho ambayo husumbua Zaidi Watu Duniani Kote,
Matatizo ya Macho huathiri watu wengi, mfano kwa Mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO);
Ulimwenguni, angalau watu bilioni 2.2 wana shida ya kuona kwa karibu au kwa umbali. Katika angalau bilioni 1 kati ya hizi, uharibifu wa kuona ungeweza kuzuiwa au bado haujashughulikiwa.
“Globally, at least 2.2 billion people have a near or distance vision impairment. In at least 1 billion of these, vision impairment could have been prevented or is yet to be addressed”.
MAGONJWA YA MACHO AMBAYO HUWAPATA WATU WENGI ZAIDI.
Haya hapa ni baadhi ya magonjwa ya macho ambayo huwapata watu wengi zaidi,
NB: Hizi namba zimeandikwa kwa ujumla lakini haimaanishi kwamba ugonjwa wa macho ulioandikwa kwanza ndyo una wagonjwa wengi Zaidi kuliko mengine,
KUMBUKA: Soma Hapa Ugonjwa wa RED EYES.
SOMA ZAIDI HAPA: ugonjwa wa RED EYES,chanzo,dalili na Tiba yake
Hii ndyo Orodha ya baadhi ya magonjwa ya macho tulioyachambua kwa Leo;
1.Ugonjwa wa Presha ya macho ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Glaucoma.
SOMA HAPA ZAIDI: Ugonjwa huu wa presha ya macho(Glaucoma)
2. Ugonjwa wa mtoto wa jicho au kwa kitaalam hujulikana kama Cataract.
Ugonjwa huu huhusisha uwepo wa kitu kama wingu kwenye lensi za macho, na ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza duniani kwa kusababisha Upofu wa macho.
SOMA HAPA ZAIDI: Ugonjwa huu wa mtoto wa jicho(Cataract)
3. Ugonjwa wa vikope maarufu kama Trakoma, kujua zaidi ugonjwa wa VIKOPE au TRAKOMA
SOMA HAPA: Ugonjwa wa vikope au Ugonjwa wa TRAKOMA,chanzo,dalili na Tiba yake
4. Ugonjwa wa RED EYES.
SOMA ZAIDI HAPA: ugonjwa wa RED EYES,chanzo,dalili na Tiba yake
5. Tatizo la Diabetic Retinopathy, shida hii hutokana na ugonjwa wa kisukari, ambapo ugonjwa huu wa kisukari huleta madhara makubwa hadi kwenye mishipa ya damu ndani ya Retina,
Na ndyo maana baadhi ya wagonjwa wa kisukari wanapatwa na tatizo la macho kutokuona vizuri pia.
6. Tatizo la Refractive Errors, ambapo huhusisha shida ya kuona karibu yaani myopia (near-sightedness), shida ya kuona mbali yaani hyperopia (farsightedness), pamoja na tatizo la macho kutokuona vizuri mbali wala karibu yaani astigmatism (distorted vision at all distances).
kwa Mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO);
Ulimwenguni, angalau watu bilioni 2.2 wana shida ya kuona kwa karibu au kwa umbali. Katika angalau bilioni 1 kati ya hizi, uharibifu wa kuona ungeweza kuzuiwa au bado haujashughulikiwa.
7. Tatizo la Age-Related Macular Degeneration, ambapo tatizo hili la macho hutokana na umri mkubwa au uzee,
8. Tatizo la Amblyopia au kwa lugha nyingine hujulikana kama Lazy Eye, Tatizo hili la macho huaathiri zaidi uwezo wa kuona kwa watoto wadogo,
Na tatizo hili hutokana na macho pamoja na Ubongo kutokufanya kazi vizuri kwa kushirikiana hali ambayo hupelekea uwezo wa kuona kwa jicho moja kupungua sana,
Na wakati mwingine tatizo la Cataract pamoja na Strabismus huchangia pia uwepo wa shida hii.
9. Tatizo la Strabismus, tatizo hili huhusisha kutokuwa na uwiano(imbalance) kwenye kuposition macho yako mawili.
Na tatizo hili hutokana na kukosa coordination kati ya macho yako mawili, na matokeo yake macho yako mawili huangalia kwenye direction tofauti, badala ya macho yote mawili kufocus kwenye kitu kimoja, kila jicho hutazama upande wake.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.