Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini?
Hili ni Swali ambalo watu wengi huuliza na wengi wao wanafahamu kama ugonjwa wa moyo ni ugonjwa mmoja, Hapana fahamu hapa…!!!
Ugonjwa wa Moyo;
Ni maneno yanayoelezea magonjwa yote yanayoathiri moyo au kwa kitaalam tunaita heart diseases, hakuna Ugonjwa mmoja wa moyo, ila kuna magonjwa mbali mbali yanayoathiri moyo.
Hivo mtu akikuambia una ugonjwa wa Moyo,muulize ugonjwa upi wa moyo?.
Mfano wa magonjwa hayo yanayoathiri moyo ni pamoja na;
- Ugonjwa unaoathiri mishipa ya damu ndani ya moyo mfano; Coronary artery diseases.
- Tatizo la mapigo ya moyo kutokueleweka-Irregular heartbeats (arrhythmias)
- Tatizo kwenye muundo wa moyo ambapo unazaliwa nalo (congenital heart defects)
- Tatizo la moyo kutanuka
- Tatizo la Moyo kujaa maji
- Ugonjwa wa kwenye misuli ya Moyo
- Ugonjwa wa kwenye Valve za moyo
- Ugonjwa wa kwenye mfumo wa umeme ndani ya moyo n.k
Dalili za Ugonjwa wa Moyo
Dalili zinategemea na aina ya Ugonjwa wa moyo unaokusumbua kwa wakati huo, Kwa Mfano;
Dalili za Ugonjwa wa Moyo unaoathiri mishipa ya damu(Coronary artery disease) ni pamoja na;
- Kupata maumivu ya kifua,kifua kuwa kizito au kubana
- Kukosa pumzi au mtu kupumua kwa shida
- Kupata maumivu ya shingo,taya, koo,sehemu ya juu ya tumbo au mgongoni
- Kuhisi hali ya ganzi kwenye viungo vya mwili,
- Viungo kama miguu au mikono kuhisi hali ya kupoa sana(baridi), kuwa dhaifu, au kupata ganzi n.k
Dalili za Ugonjwa wa moyo kutokana na shida ya mapigo ya moyo kutokuelewe irregular heartbeats (heart arrhythmias);
- Kupata maumivu ya kifua
- Kuhisi hali ya kizunguzungu
- Kuzimia
- Kuhisi maumivu ya kichwa
- Kupata shida ya mapigo ya moyo kwenda mbio zaidi (tachycardia)
- Kupata shida ya mapigo ya moyo kwenda taratibu(bradycardia)
- Mtu kukosa pumzi au kupumua kwa shida n.k
Dalili za Ugonjwa wa Moyo kutokana na hitilafu uliyozaliwa nayo(congenital heart defects);
- Ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa kijivu au blue (cyanosis)
- Kuvimba miguu,tumbo au kuzunguka macho
- Kukosa pumzi au kupumua kwa shida n.k
Dalili za Ugonjwa wa Moyo kutokana na shida kwenye misuli ya Moyo: heart muscle (cardiomyopathy);
- Kupata kizunguzungu
- Mwili kuchoka kupita kiasi
- Kupumua kwa shida baada ya kufanya kazi kidogo au hata ukiwa umepumzika
- Mapigo ya moyo kwenda mbio sana
- Kuvimba miguu,mikono n.k
Ugonjwa wa moyo husababishwa na nini?
Zipo sababu mbali mbali kulingana na aina ya Ugonjwa wa moyo, na Sababu hizo ni pamoja na;
– Kuwa na makovu kwenye misuli ya Moyo(Heart muscle scarring),
Hii inatokana na Sababu mbali mbali ikiwemo: kuumia/kupata ajali na kuwa na kidonda kwenye moyo n.k
– Kuwa na mafuta yanayosababisha kuziba kwenye mishipa ya damu ndani ya moyo(Coronary artery disease)
– Matatizo ya kurithi(Genetic issues).
– Kuwa na Matatizo kwenye Utendaji kazi wa Figo
– Maambukizi ya magonjwa mbali mbali, hapa tunazungumzia mtu kushambuliwa na viini mbali mbali vya magonjwa ikiwemo;
- Bacteria
- Fangasi
- Virusi n.k
– Kuwa na matatizo kwenye tezi la Thyroid(Thyroid problems).
– Kuwa na magonjwa kama vile Rheumatic disease.
– Kuumia Sehemu ya moyo
– Kuwa na Shida ya shinikizo la Juu la Damu(High blood pressure)
– Kupata Shida ya Shambulio la Moyo(Heart attacks)
– Matumizi ya baadhi ya Dawa, mfano baadhi ya dawa za chemotherapy n.k
– Kuwa na magonjwa jamii ya Autoimmune diseases. n.k.
Vitu hizi huongeza hatari ya Mtu kupata Ugonjwa wa Moyo?
- Kuwa Mzee
- Kuwa na kiwango cha juu cha cholestrol kwenye damu
- Kuwa na shinikizo la juu la damu
- Matumizi ya tumbaku au Uvutaji wa Sigara
- Unywaji wa Pombe
- Kuwa na Uzito mkubwa wa mwili
- Kutokufanya Mazoezi
- Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari
- Kula vyakula vya mafuta mengi,chumvi nyingi n.k
Vipimo unavyoweza kufanya ili kugundua Ugonjwa wa Moyo ni pamoja na;
– Electrocardiogram (EKG or ECG).
– Ambulatory monitors.
– Echocardiogram (Echo).
– Cardiac computerized tomography (CT).
– Heart magnetic resonance imaging (MRI).
– Vipimo vya Damu(Blood tests) n.k
Matibabu ya Ugonjwa wa Moyo
Matibabu ya Ugonjwa wa Moyo yanategemea chanzo husika pamoja na aina ya Ugonjwa wa moyo, ila kwa Ujumla kuna;
- Dawa
- Upasuaji
- Pamoja na kubadilisha kabsa mtindo wa maisha
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Bonus Tips; Zingatia Mambo Haya Muhimu;
✓ Hakikisha unadhibiti Uzito wako wa mwili, na kuwa na Uzito unaotakiwa kiafya
✓ Hakikisha unakula mlo bora kiafya(Healthly diet)
✓ Jitahidi kufanya Mazoezi ya mwili angalau kwa Nusu Saa(dakika 30) kila siku
✓ Epuka Uvutaji wa Sigara au matumizi ya tumbaku au dawa zozote za kulevyia
✓ Epuka Matumizi ya Pombe n.k…!!!!