Umri sahihi kwa mwanaume kupata watoto
Sote tunafahamu mipaka ambayo hedhi inaweka kwenye uwezo wa kuzaa wa mwanamke, lakini labda hatujali sana kile kinachotokea kwa uzazi wa kiume baada ya umri wa kati.
Wanaume kwa kawaida huwa hawaachi kutoa mbegu za kiume lakini hiyo haimaanishi kuwa hawana ‘ukomo’ kama wanawake. Kadiri mtu anavyozeeka, mbegu zake hupitia mabadiliko ya kijeni ambayo huongeza uwezekano kwamba DNA ya manii yake inaweza kuharibika. Hii inaweza kuathiri uzazi na pia kuleta athari zinazoweza kuathiri afya ya watoto wake wa baadaye.
Uchunguzi umeonyesha kwamba akina baba wenye ‘umri mkubwa’ wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata watoto wenye matatizo ya ukuaji wa neva. Utafiti uliofanywa mwaka 2010 ulibaini kuwa watoto wa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 40 walikuwa na hatari mara tano ya kupata Hali ya Usonji (Autism Spectrum Disorder).
Ni kipindi kipi kinafaa kwa mwanaume kupata Watoto?
Umri ambao mwanaume anaweza kuwa na uzazi mkubwa zaidi ni kati ya miaka 22 na 25. Inapendekezwa kuwa na watoto kabla ya kufikia umri wa miaka 35. Baada ya umri huu, uzazi wa kiume huanza kudhoofika.
Baada ya miaka 35, manii inaweza kusababisha ujauzito ambapo mabadiliko yanaweza kutokea. Zaidi ya hayo, ikiwa umri wa mwanaume ni zaidi ya miaka 45, basi nafasi za kutokea kwa mimba kuharibika ni kubwa zaidi, bila kujali umri wa mwanamke mwenye mimba.
Kwa nini akina baba wanapata watoto katika umri mkubwa kuliko walivyokuwa zamani?
Kuna hatari gani za kuwa baba ukiwa na umri mkubwa?
Je, ni matatizo gani unakumbana nayo kwa kuwa mama katika umri mkubwa?
Umri ambao watu wanakuwa wazazi umekuwa ukiongezeka kwa kasi tangu katikati ya miaka ya sabini na sasa uko juu sana, na wastani wa umri wa baba ni miaka 34, ikilinganishwa na miaka 31 kwa akina mama.
Kwa vile wazazi wa kiume mara nyingi huwa tegemezi kwa wenzi wa kike – kwa kawaida wenye umri sawa – kushika mimba, ongezeko hili linaongezeka kwa wanaume kama inavyokua kwa wanawake pia. Lakini kama mtaalamu wa masuala ya uzazi Sarah Martins Da Silva kutoka Chuo Kikuu cha Dundee anavyobainisha, sababu kwa nini wazazi – wa jinsia yoyote – kuendelea kupata watoto katika umri mkubwa ni nyingi.
“Nadhani kuna majadiliano makubwa zaidi ya kijamii na kiuchumi karibu na hayo na ni wazi yanahusiana na uchumi, utoaji wa huduma ya watoto na watu kutokuwa na utulivu wa kifedha,” anasema.
Je mwanaume anaweza kuwa baba katika umri wowote?
Kinadharia, ndiyo, kutokana na kwamba inachukua tu manii moja yenye afya ili kurutubisha yai. Kulingana na Martins da Silva, hakuna “hatua ya kuisha kwa manii” katika hatua yoyote.
“Kuna watu maarufu wenye umri wa miaka sabini na themanini ambao wanazaa watoto,” anasema. “Na haipaswi kuwa mshangao hasa kwetu kwamba wanaume bado wanaweza kufanya hivyo, kwa sababu biolojia ni tofauti kabisa [kuliko kwa wanawake].” lakini kuna hatari zake.
Je, kuna hatari zozote zinazohusiana na kuwa baba katika umri mkubwa?
kwa bahati mbaya, kuna hatari zilizoongezeka kwa baba na watoto wanaozaliwa katika umri mkubwa. Tathmini ya 2020 iliyoangalia athari za umri wa baba katika kuharibika kwa mimba, iligundua kuwa hatari ya kuharibika kwa mimba huongezeka kwa umri, ingawa madhara ya umri wa kike katika kupoteza mimba yanaonekana ni makubwa zaidi.
Kwa watoto wanaozaliwa na baba wenye umri mkubwa, kuna ushahidi mwingi unaoonyesha wako katika hatari kubwa ya kupata aina mbalimbali za matatizo ya kiafya, ambazo zinaweza kuhusishwa na mabadiliko ya kijeni yanayojiri kadri tunavyozeeka. Kasoro za moyo hutokea mara nyingi zaidi na hatari ya magonjwa ya akili huongezeka kwa watoto walio na baba wenye umri mkubwa.
Athari nyingine huwa za kijamii, watoto wengi walio na baba wenye umri mkubwa wanakabiliana nayo, ni baba yao kufariki wakiwa bado wachanga na athari zozote zinazoweza kuwa nazo.
“Wanaelekea kufanya vibaya zaidi katika suala la maendeleo ya kijamii, maendeleo ya shule na kadhalika,” anasema Martens da Silva. “Lakini mara nyingi huwa katika hali ambayo kuna shida nyingi za kifedha pia.”
Mtindo wa maisha na athari zake
Kuna mambo mengi ya mtindo wa maisha yanayoweza kudhoofisha ubora wa manii. Haya ni pamoja na lishe duni, uvutaji wa sigara, kunywa pombe, kutumia dawa za kulevya, na unene wa kupindukia.
Kusafiri kwa manii ni uwezo wa manii kuhamia kwa ufanisi kupitia njia ya uzazi ya mwanamke ili kufikia na kurutubisha yai. Uvutaji wa sigara umeunganishwa sio tu na kupungua kwa ubora wa manii, bali pia na idadi na kasi ya manii kuelekea kwenye yai.