Upungufu wa protini mwilini husababisha ugonjwa gani
Kuna aina kuu mbili za matatizo yanayotokana na upungufu wa protini mwilini ambapo ni;
- Kwashiorkor
- Marasmus.
Kwashiorkor huathiri mamilioni ya watoto duniani kote. Ilipotajwa kwa mara ya kwanza mnamo 1935, zaidi ya asilimia 90 ya watoto walio na Kwashiorkor walikufa. Ingawa vifo vinavyohusishwa na kwashiorkor ni vya kiwango cha chini kidogo kwa sasa, watoto wengi bado wanakufa baada ya kuanza kwa matibabu.”
Protini ni mjenzi mkuu wa misuli yako, ngozi, vimeng’enya(enzymes) na homoni, na ina jukumu muhimu katika tishu zote za mwili.
Upungufu wa proteins husababisha matatizo mbalimbali ya afya, Takwimu zinaonyesha watu takribani million Moja duniani kote wanatatizo la kutokupata protini ya kutosha,
Na Tatizo ni kubwa zaidi katika Afrika ya Kati na Kusini mwa Asia, ambapo hadi asilimia 30% ya watoto hupata protini kidogo kutoka kwenye lishe yao.
Baadhi ya Watu katika nchi zilizoendelea pia wako katika hatari. Hii ni pamoja na watu wanaofuata lishe isiyo sawa(imbalance diet), na vile vile wazee na wagonjwa waliolazwa hospitalini.
Dalili za kwashairokor
Upungufu wa Proteins huweza kuleta Matatizo haya;
1. Kudhoofika kwa misuli ya Mwili
2. Kuvimba kama dalili mojawapo ya kwashiorkor
3. Kupata tatizo la Fatty Liver,
Tatizo ambalo huhusisha mafuta kujikusanya kwenye seli za Ini
4. Kupata matatizo ya ngozi, nywele na kucha,
Kwa mfano, kwashiorkor kwa watoto inaweza kusababisha ngozi kuwa dhaifu au kupasuka, uwekundu na mabaka mabaka ya ngozi, ngozi kubadilika rangi.n.k
Nywele kuwa nyembamba zaidi kunyonyoka haraka, kuwa na rangi ya nywele iliyofifia, upotezaji wa nywele (alopecia) na kucha zilizovunjika pia ni dalili za kawaida sana kutokea kwa mgonjwa.
5. Kuwa kwenye hatari kubwa ya kuvunjika kwa mifupa,
Misuli siyo tishu pekee zinazoathiriwa na upungufu wa proteini mwilini hata Mifupa pia,
Kutotumia protini ya kutosha kunaweza kudhoofisha mifupa yako na kuongeza hatari ya kuvunjika.
6. Tatizo la Udumavu kwa Watoto,
Proteins ni muhim pia kwa ukuaji wa mwili, hivo watoto wenye upungufu wa proteins huathiriwa ukuaji wao pia au hudumaa.
7. Kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa,
Fahamu upungufu wa proteins pia huathiri mfumo wa kinga ya mwili, hali ambayo huongeza hatari ya mwili kushambuliwa.
Utendaji dhaifu wa kinga ya mwili unaweza kuongeza hatari au ukali wa maambukizi, Hii ni dalili nyingine ya upungufu mkubwa wa protini.