Telepathy: Chipu ya ubongo ambayo Elon Musk anadai aliiweka ndani ya mwanadamu inaleta mashaka gani?
Kampuni ya Musk haiko peke yake katika kinyang’anyiro cha chipu za ubongo zisizotumia waya.
Je, siku inakaribia ambapo wanadamu wataweza kudhibiti kompyuta kwa kutumia akili zao?
Mjasiriamali Elon Musk alichochea mjadala huo kwa kutangaza siku ya Jumatatu kwamba kampuni yake ya Neuralink ilifanikiwa kupachika moja ya chipu zake za ubongo ndani ya binadamu.
Katika chapisho kwenye X, Elon Musk alisema kuwa shughuli za “kuleta matumaini” za ubongo ziligunduliwa baada ya kuwekewa chipu hizo na kwamba mgonjwa “amepona vizuri.”
Lengo la kampuni ni kuifanya teknolojia iwe yenye kufaa kwa ajili ya kutibu magonjwa magumu ya neva.
“Kwa kampuni yoyote inayotengeneza vifaa vya matibabu, jaribio la kwanza la mwanadamu ni hatua muhimu,” anasema Profesa Anne Vanhoestenberghe kutoka taasisi ya King’s London.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, makampuni kadhaa yanafanyia kazi bidhaa zinazotia matumaini , lakini ni machache tu ambayo yamefanikiwa kuingiza vifaa vyao kwa binadamu.
Vanhoestenberghe anaonya, hata hivyo, kwamba “mafanikio ya kweli” yanaweza kupimwa kwa muda mrefu tu na kwamba “Elon Musk ni mzuri sana katika kuchochea hisia kuhusu kampuni yake.”
Hadi sasa, hakuna uthibitisho wa kujitegemea wa madai ya Musk. Neuralink pia haikutoa taarifa kuhusu utaratibu huo.
BBC imewasiliana na kampuni hiyo na mdhibiti wa matibabu wa Marekani, Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA), kwa maoni.
Jinsi Telepathy inavyofanya kazi?
Katika chapisho lingine kwenye X, Musk alionyesha kuwa bidhaa ya kwanza ya Neuralink itaitwa Telepathy.
“Watumiaji wa kwanza watakuwa wale ambao wamepoteza udhibiti wa viungo vyao,” aliongeza Bw. Musk.
Kisha akamtaja Stephen Hawking, mwanasayansi maarufu wa Uingereza ambaye aliugua ugonjwa mbaya wa ubongo.
“Fikiria kama mchuuzi angeweza kuwasiliana haraka kuliko dalali. Hilo ndilo lengo.”
Utaratibu huo unahusisha kupandikiza chipu ndogo, iliyofungwa kwa kifaa hermetically moja kwa moja kwenye ubongo wa mgonjwa.
Chipu hii imeunganishwa kwa vifaa vidogo vya kielekroniki 1,024, vyenye ukubwa ulio sawa na ywele za binadamu, na kinaendeshwa na betri inayoweza kuchajiwa bila waya.
Kifaa hiki kinawasiliana na kompyuta ya nje, ikiruhusu kutuma na kupokea ishara.
Je, lenzi ya Neuralink iko salama?
Kampuni kadhaa zimeingia katika matumizi ya matibabu ya vipandikizi vya chip za ubongo.
Wasiwasi kuhusu teknolojia hii ni pamoja na hatari za kimwili za muda mfupi, athari za muda mrefu za matibabu na maswali ya kimaadili.
Uendeshaji wowote wa ubongo hubeba hatari.
Mnamo Disemba 2022, ripoti ya Reuters ilionyesha kuwa Neuralink ilishiriki katika majaribio ambayo yalisababisha vifo vya takriban wanyama 1,500, wakiwemo kondoo, nyani na nguruwe.
Mnamo Julai 2023, Idara ya Kilimo ya Marekani, ambayo ina jukumu la kuchunguza masuala ya ustawi wa wanyama, ilisema haikukubaini ukiukwaji wowote wa sheria za utafiti wa wanyama katika kampuni ya Musk, ingawa uchunguzi tofauti unaendelea.
Ukweli kwamba FDA iliidhinisha majaribio ya kibinadamu, hata hivyo, ina maana kwamba kampuni ya Musk imeshinda baadhi ya vikwazo vyake.
Labda wasiwasi mkubwa zaidi ni matokeo ya muda mrefu ya kutumia kifaa kama hicho kwenye ubongo, chombo kigumu ambayo bado hayajajulikana.
Kwa vile hii ni tasnia changa, hakuna data za kutosha kuhusu madhara yanayoweza kutokea. Hii itabadilika na majaribio ya kibinadamu na itakuwa muhimu kwa maendeleo ya bidhaa zinazofanana.
Maswali ya kimaadili ni ya kibinafsi zaidi. Teknolojia hizi huibua wasiwasi kuhusu ulinzi wa data, matumizi yanayowezekana na uwezekano wa kuimarisha uwezo wa utambuzi wa binadamu.
Miradi mingine
Nchini Uchina, kituo kimejitolea pekee kwa utafiti na uvumbuzi katika uwanja wa ujumuishaji wa ubongo na kompyuta.
Wakati teknolojia ya Musk ikijadiliwa kufuatia tangazo lake, baadhi ya wapinzani wake wamekuwa na teknolojia hii miongo miwili.
Kampuni ya Marekani ya Blackrock Neurotech, yenye makao yake makuu katika jimbo la Utah, ilitekeleza njia ya kwanza kati ya nyingi za kompyuta za ubongo mwaka wa 2004.
Precision Neuroscience, iliyoundwa na mmoja wa waanzilishi-wenza wa Neuralink, pia inalenga kusaidia watu waliopooza.
Kipandikizi chake kinaonekana kama kipande chembamba cha mkanda ambacho huwekwa kwenye uso wa ubongo na kinaweza kupandikizwa kupitia “cranial microslit,” ambayo kampuni inasema ni utaratibu rahisi zaidi.
Vifaa vingine vilivyopo pia vimetoa matokeo.
Katika tafiti mbili tofauti za kisayansi zilizofanywa hivi karibuni nchini Marekani, vipandikizi vilitumiwa kufuatilia shughuli za ubongo wakati mtu alipojaribu kuongea, shughuli ambayo inaweza kuamuliwa ili kuwasaidia binadamu katika mawasiliano.
Makampuni mengine yamefanya maendeleo sawa katika eneo hili, ikiwa ni pamoja na École Polytechnique Fédérale de Lausanne (EPFL) ya nchini Uswisi, ambayo iliweza kumwezesha mtu aliyepooza kutembea kwa kufikiri tu.
Ili kufanya hivyo, vipandikizi vya kielektroniki viliwekwa kwenye ubongo na uti wa mgongo wa mwanamume huyo ili kuwasilisha mawazo yake bila waya kwenye miguu yake.
Maelezo ya awali ya maendeleo ya utafiti huu yalichapishwa katika jarida lililopitiwa na jarida la tathimini ya uvumbuzi wa kisayansi – Nature, mnamo mwezi Mei 2023.