Fahamu Uvimbe mwilini unaweza kusababisha magonjwa katika mfumo wa usambazaji wa damu kwenye ubongo.
Katika makala hii tunachambua Jinsi Uvimbe wa kudumu unavyoweza kuathiri vibaya afya yako(inflammation);
Kwa kawaida wakati umepata maambukizi, jeraha,sumu kuingia mwilini au kwa ujumla kitu hatari ambacho kinaweza kudhuru mwili wako; uchochezi hutokea kama mchakato katika mwili wako wa kupigana na vitu hivi, Hii ni kama njia ya mwili kujiponya wenyewe,
Katika mchakato huu, mwili hutoa kemikali kama vile kingamwili au protini na kuongezeka kwa mtiririko wa damu kwenye eneo lililoharibiwa, jambo ambalo huchochea mwitikio wa utendaji wa mfumo wako wa kinga ya mwili.
Hivi ndivyo inavyotokea tunapojikata, kwa mfano. Eneo lililoathiriwa mara moja huwasha, hugeuka rangi na kuwa jekundu na tunaweza kuhisi maumivu, kisha mwili huchukuliwa hatua kwa hatua(process) mpaka unapojiponya wenyewe.
Na mwitikio huu wa mwili wa haraka na wa muda mfupi katika kujiponya, ndyo huleta matokeo ya kama Uvimbe (Inflammation) usio na madhara makubwa mwilini,
Na Kusudi kubwa ni kuulinda mwili, pamoja na kuondoa vijidudu vinavyovamia ambavyo vinaweza kuwa na madhara,
Katika hali hyo,ndipo mwili huanza kupata Ishara na Dalili mbali mbali ikiwemo;
- Kupata homa
- Mafuta
- Maumivu ya kichwa
- Ngozi kuwasha
- Kuvimba n.k
Kuvimba ikiwa kama matokeo ya kinga ya mwili dhidi ya mapambano ya vitu mbali mbali kama vile; maambukizi,majeraha n.k, kunaweza kuwa na athari hasi mwilini hasa ikiwa ni Uvimbe wa Muda Mrefu.
Ikiwa una uvimbe mwilini (inflammation) kwa muda mrefu , inaweza kuwa hatari, kwa sababu uvimbe huu unahusishwa na kupoteza kazi ya michakato mingi ya kisaikolojia na kiakili.
Uvimbe wa muda mrefu usiodhibitiwa utakuza aina zote za magonjwa au maambukizo sugu kama vile saratani, mizio(allergies) na magonjwa mengine kama vile pumu na ukosefu wa kinga ya mwili,”.
Pia, wataalam wanatoa maoni, magonjwa kama vile kuharibika kwa mimba, kuathiriwa kwa mfuko wa uzazi au kuharibika kwa kiinitete,vyote hivi huweza kuwa matokeo ya Uvimbe(Uvimbe wa kizazi).
Pia,Fahamu Uvimbe mwilini ukiwa wa kudumu unaweza kusababisha magonjwa katika mfumo wa usambazaji wa damu kwenye ubongo.
Mnamo mwaka wa 2018, jarida la Nature lilichapisha utafiti ambao ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 50% ya vifo vyote ulimwenguni vinatokana na magonjwa yanayohusiana na uchochezi: kuanzia ugonjwa wa moyo wa ischemic, ambo hutokea wakati mishipa inayosambaza damu kwenye misuli ya moyo inakuwa imeziba, saratani, kisukari, na magonjwa mengine ya ukosefu wa kinga mwilini.
Kwa nini kuvimba mwilini (Inflammation) hutokea kwa muda mrefu?
Kuvimba kunaweza kuwa kwa Muda mrefu kwa sababu maambukizi bado yapo au jeraha halijapona vizuri,
Jambo jingine ambalo linaweza kusababisha uvimbe kuendelea kuwepo ni wakati una ugonjwa wa autoimmune, ambapo mfumo wa kinga hushambulia vibaya tishu zenye afya au mfumo wa mwili kwa ujumla.
Huweza pia kusababishwa na hewa chafu au kemikali za viwandani.
Na kutokana na mabadiliko makubwa kwenye maisha ya binadamu tangu miaka 50 iliyopita,
‘’ Tunakula vyakula vilivyosindikwa zaidi, vitu vingi ambavyo ni vibaya kwa afya yetu. Na hivyo uwiano kati ya bakteria wazuri na bakteria nyemelezi hukosekana”, anasema Dkt . Alecsandru.
‘’Kulala muda mfupi , kuwa na mafadhaiko makubwa au Msongo wa mawazo(stress) pia hupunguza sana mwitikio wa kinga, kuvuta sigara, kunywa pombe, kula vibaya au kula vyakula vya mafuta mengi, na ukosefu wa vitamini D itokanayo na jua huathiri utendaji mzima wa mwili na kusababisha uvimbe mwilini (inflammation)’’, anasema.