Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO
Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi yake ya Asili, na kukufanya uwe na mabaka mabaka.
Dalili za Ugonjwa wa Ngozi kuwa Nyeupe,Vitiligo
Dalili ya Ugonjwa huu wa Vitiligo ni pamoja na;
✓ Ngozi kuanza kupoteza rangi yake ya asili na kuwa na mabaka mabaka ambapo kwa asilimia kubwa, mara ya kwanza huanza kuonekana maeneo kama vile;
- Mikononi
- Usoni
- Sehemu Za Siri
- Na maeneo yote ya mwili karibu na tundu au uwazi
✓ Nywele kuwa nyeupe au kuwa kama Mvi kwenye maeneo ya Kichwani,Kope,nyusi,au Ndevu n.k
✓ Kupotea kwa rangi ya asili kwenye Tishu ambazo zinazunguka Mdomo,Lips za mdomo,Puani n.k
Ugonjwa wa Vitiligo unaweza kuanza kwenye Umri wowote ingawa mara nyingi huanza kabla ya Mtu kufikisha Umri wa miaka 30.
Chanzo cha Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO
Ugonjwa wa Vitiligo hutokea pale ambapo seli zinazozalisha rangi (melanocytes) kufa au kuacha kabsa kuzalisha melanin — ambapo hii ndyo pigment inayoipa ngozi rangi,nywele pamoja na macho.
Vipande vinavyohusika vya ngozi huwa vyepesi au vyeupe. Haijulikani ni nini hasa husababisha seli hizi za rangi kushindwa kufanya kazi au kufa. Ingawa Inaweza kuhusishwa na sababu mbali mbali ikiwemo:
- Matatizo ya Mfumo wa Kinga ya Mwili (autoimmune condition)
- Matatizo ya Urithi,Family history (heredity)
- Matukio kama vile kuungua sana kwenye ngozi
- Kuumia sana au kupata majeraha makubwa ya Ngozi baada ya kugusana na baadhi ya Kemikali
- Msongo wa mawazo n.k
Kumbuka; Melanin ni natural pigment ambayo huipa ngozi rangi yake ya asili, na huzalishwa na Seli zinazojulikana kama melanocytes.
Vitu ambavyo huongeza hatari ya Kupata Ugonjwa wa Vitiligo
– Kuwa na Mtu mwenye shida hii kwenye Familia yako
– Kuwa kwenye mazingira ya kugusa kemikali mara kwa mara,mfano phenol-containing chemicals,n.k
– Kupata matukio kama vile kuungua sana Ngozi, kupata majeraha makubwa ya ngozi n.k
– Kuwa na matatizo kwenye Mfumo wa kinga ya Mwili n.k
Fahamu Pia,Mtu mwenye Ugonjwa wa Vitiligo huweza kupata madhara mengine ikiwemo;
- Kuathirika kisaikolojia
- Kuungua sana ngozi jua likimchoma
- Kuwa na Matatizo ya Macho
- Kuwa na tatizo la kupotea kwa Usikivu n.k
FAHAMU KWA KINA TATIZO AU UGONJWA WA VITILIGO (UGONJWA UNAOIFANYA NGOZI KUPOTEZA RANGI YAKE)
• • • • • •
Ni tatizo linaloifanya ngozi ipoteze rangi yake ya asili. Sehemu zinazopoteza rangi huongezeka ukubwa kadri siku zinavyozidi kwenda. Tatizo hili linaweza kuathiri pia nywele,pamoja na sehemu ya ndani ya kinywa
Siku zote rangi ya ngozi na nywele za binadamu huamuliwa na vichocheo vya melanin. Vitiligo hutokea baada ya sehemu (seli) zinazozalisha vichocheo ya melanin kufa,au vikiacha kufanya kazi. Kwa msingi huu,kufa au kuacha kufanya kazi kwa seli zinazozalisha melanin kunaweza kusababishwa na mambo matatu
1.Matatizo kwenye mfumo wa ulinzi wa mwili ambao huanza kuzishambulia seli zake wenyewe kama maadui (wavamizi),jambo ambalo kitaalamu huitwa Autoimune condition
2.Kurithi
3.Mzio (allergy),stress pamoja na mionzi mikali ya jua au ajali kubwa ya ngozi
Tatizo hili siyo la kurogwa wala kuambukizwa,na haliwezi kumpata mtu mwingine kwa kugusana au hata kushirikiana naye mambo kadhaa kwenye jamii,hivyo tusiwatenge na kuwanyanyapaa wagonjwa wa tatizo hili ambao hupitia kipindi kigumu sana cha masongo wa mawazo,kuungua vikali na mwanga wa jua pamoja na matatizo ya kuona na kusikia
Tatizo hili halina tiba ya kudumu,hata hivyo msaada wa matibabu hutolewa kulingana na umri,ukubwa wa tatizo,jinsi maisha ya mtu yalivyo athirika pamoja na kasi ya kukua kwa tatizo.
Vyote hivi hulenga kuleta ahueni ya tatizo kwa mgonjwa pamoja na kuipunguza kasi ya kukua/kusambaa kwa tatizo hili.