Chanzo cha Kutokwa na malengelenge mwilini
Kutokwa na malenge mwilini ni neno linalomaanisha kutokwa na upele kwenye ngozi ambao ukipasuka au kupasuliwa hutoa majimaji.
Vipele vya malenge kwa jina jingine hufahamika kama vipele maji. Sifa ya vipele hivi ni kuwa na kipenyo chini ya sentimita 0.5, vyenye mipaka ya kueleweka na hutokea kimoja au kwenye kundi.
Wakati mwingine haraha hizi kutokea pamoja na upele mkubwa wenye maji kwa jina la bullae(lenge kubwa). Bullae ni lenge kubwa lenye kipenyo cha zaidi ya sentimita 0.5.
Vipele maji huweza kutokea vichache au vingi na pia huweza kudumu kwa muda mfupi au kuwa sugu.
Kuna sababu nyingi zinaweza kuchangia kupata vipele maji kwenye ngozi kama vile, michomo, mwitikio wa mzio, madhaifu ya umetaboli wa molekyuli mbalimbali mwilini na maambukizi kwenye ngozi.
Visababishi vya Malengelenge
Malenge ya kuungua
Michomo ya ngozi daraja la pili mara nyingi huzalisha malenge ya maji mwilini. Michomo huu huathiri ngozi ya juu na sehemu kidogo ya ngozi ya chini, hii hupelekea kutokea kwa malengo madogo au makubwa pamoja na dalili zingine kama, maumivu, wekundu kwenye ngozi, na unyevuunyevu kwenye eneo lililoungua.
Malenge ya ugonjwa wa Demataitiz ya mguso
Kwa sababu ya kutokea kwa mwitikio wa kinga za mwili kwenye mzio wa ngozi, mzio huu huzalisha malengelenge madogo kwenye ngozi yaliyozungukwa na wekundu kwenye mipaka yake na uvimbe. malenge yanaweza kupasuka na kutoa maji, kutengeneza magamba na kusababisha muwasho.
Malenge ya Dermatitis herpetiformis
Ni ugonjwa wa ngozi unaotokea sana kwa wanaume kati ya umri wa miaka 20 hadi 50. Ugonjwa huu wakati mwingine huhusiana na ugonjwa wa celiac, saratani ya maungo ya ndani ya mwili na matibabu ya kutumia immunoglobulin A. Malenge yanayozaliswha kutokana na ugonjwa huu huwa sugu, huweza kuwa makubwa , yenye usaha au kuwa na ugumu kama vilele vidogo. Mara nyingi vipele hivi hutokea kwa mpangilio unaofanana na pande mbili za mwili mfano kwenye makalio, magoti, usoni, kichwani na shingoni. Dalili zingine ni pamoja na muwasho mkali, hisia za kuungua na kung’atwa. Baadhi ya malenge yanaweza kutoa usaha na majimaji yenye rangi ya damu iliyooza.
Malenge ya Erithima matifomu (Erythema multiforme)
Erithima matifomu ni michomo ya muda mfupi itonanayo na kinga za mwili kwenye ngozi inayoambatana na mabaka mekundu, upele mdogo na wakati mwingine upele malenge makubwa yaliyo na maji ndani. Magamba ya erithima matifomu huonekana kwenye ngozi ya maeneo mikono, viganja vya mikono, miguu, uso na shingo. Vipele huweza tokea na kupotea na kutokea tena wakati mwingine. Licha ya kuweza kutokea sehemu yoyote ya mwili, malenge madogo na makubwa huonekana sana kwenye maeneo ya ngozi laini haswa kwenye midomo na ndani ya kinywa, yanaposuka hutegeneza vidonda na kuzalisha ute mzito wenye rangi ya njano au nyeupe. Makovu yanayotoa damu, na majimaji yanayonuka huweza ambatana na dalili ya kushindwa kutafuna au kumeza chakula pamoja na kuvimba mitoki ya maeneo ya shingo.
Malenge ya maambukizi ya kirusi cha Herpes simplex.
Maambukizi ya kirusi Herpes simplex ni kawaida sana kusababisha malenge yaliyo kwenye mkusanyiko kwenye maeneo ya midomo na sehemu ya chini ya uso. Asilimia 25 ya wagonjwa wa kirusi huyu, huwa na malenge pia kwenye maeneo ya siri. Sifa ya vipele hivi huwa vinawasha, vinachomachoma, kuleta hisia za kuungua na huwa kwenye makundi au kimoja kimoja na huwa na kipenyo cha milimita 2 hadi 3 na huwa haviungani kutengeneza upele mmoja mkubwa. Upele unapopasuka hutengeneza kidonga kinachouma na kufuatiwa na kufanyika kwa gamba gumu juu ya kidonda.
Malenge ya kung’atwa mdudu
Malenge ya kung’atwa na mdudu huanza kwa kuleta wekundu kwenye ngozi kisha kuzuka kwa vipele ambavyo vinaweza kutoa damu.
Malenge ya maambukizi ya tibea pedis
Tinea pedis. Tinea pedis ni maambukizi ya fangasi kanyagio na katikati ya vidole, fangasi hawa huweza sababisha malenge kwenye maeneo tajwa na baadaye hubadilika na kuwa magamba. Maambukizi makali huambatana na michomo, muwasho na kushindwa kutembea.
Malenge ya skabi.
Huzalisha malenge madogo enye shina jekundu kwenye miishio ya shimo lililotobolewa na mdudu. Tundu huwa na urefu wa sentimita chache na huwa na uvimbe wa sentimita moja au zaidi au upele mdogo mwekundu wenye mdudu mdogo (Sarcoptes scabiei)
Chunusi kubwa zenye usaha pamoja na magamba yanaweza kutokea. Wadudu wanaweza kuchimba mashimo kwenye kichwa cha uume, mpini wa uume na kwenye ngozi iliyoshika korodani kwa wanaume na hujichimbia kwenye titi la mwanamke pia. Sarcoptes scabiei huweza kujichimbia pia katikati ya vidole, maungio ya kiganja cha mkono na mkono, maungio ya mkono wa mbele na mkono, kwapani na maeneo ya kiuno kwa jinsia yoyote ile. Ugonjwa huu huleta dalili ya muwasho inayoongezeka zaidi kwenye kipinid cha joto na haswa wakati wa usiku.
Malenge ya Surua.
Surua kwa jina jingine la kitiba smallpox, huanza kuonekana na dalili ya homa kali, uchovu wa mwili, mwili kulegea, maumivumakali ya kichwa, maumivu ya mgongo na maumivu ya tumbo. Harara bapa au upele mdogo huanza kutokea kwanza kwenye maeneo ya ngozi laini ya midomo, koo, uso na mkono wa mbele na baadae kusambaa kwenye kiwiliwili na miguuni. Ndani ya siku 2 harara hubadilika na kuwa malenge na baadae kujaa usaha. Upele hutokea kwa wakati mmoja, hufanana na huonekana sana kwenye maeneo ya uso na miishio ya mwili. Upele wenye usaha huwa na umbo duara, mgumu na shina lililozama chini ya ngozi. Baada ya siku 8 hadi 9, upele wenye usaha hutengeneza gamba, baadaye hudondoka na kuacha kovu lenye shimo. Endapo ugonjwa ni mkali yaani umehusisha ubongo, kifo hutokea, hata hivyo madhara ya ugonjwa mkali ni pamoja na kupata maambukizi ya bakteria kwenye vidonda au kupoteza damu nyingi.
Malenge ya epidemo nekrosis ya sumu
Epidemo nekrosis ya sumu (Toxic epidermal necrolysis) hutokana na mwitikio wa kinga za mwili kwenye dawa au sumu iliyoingia mwilini. Mwitikio huu huzalisha malenge makubwa kwenye ngozi yanayoanza kama mabaka yenye rangi nyekundu yakifuatiwa na kuungua , kufa kwa eneo kubwa la ngozi na kubanduka kwa ukuta wa juu ya ngozi.
Dalili zinazojitokeza ni malenge makubwa yanayopasuka na kutoa maji kwenye ngozi laini, hisia za kuungua moto kwenye konjaktiva, uchovu wa mwili, homa, na maumivu ya ngozi sehemu kubwa ya mwili. Lenge kubwa hupasuka kirahisi na kuacha ngozi wazi.
Malenge ya pofria kyutinia tada
Pofria kyutinia tada (Porphyria cutanea tarda) . Tatizo hili hutokana na madhaifu ya umetabolism wa molekuli ya porphyrin mwilini. Malenge makubwa hutokea kwenye maeneo ambayo yanapigwa na jua, yenye msuguano, majeraha au kupata joto napia husababisha dalili ya macho kuumizwa na mwanga. Machanganyiko wa Vipele vidogo vigumu au vyenye maji hubadilika kuwa vidonda na baadae makovu. dalili sugu zinazoweza kutokea ni kama vile kupauka au kutengeneza baka jeusi kwenye ngozi, kuota nywele nyingi zisizotegemea umri au jinsia(haipatrikosis), ngozi ya sklerodemoidi pamoja na kukojoa mkojo wenye rangi ya pinki au kahawia
Malenge ya ugonjwa wa Pemphigoid
Hutanguliwa na dalili za muwasho sehemu kubwa ya mwili, kuvimba kwa mwili na dalili za pumu ya ngozi kabla ya kupata malenge makubwa. Sifa za malenge huwa ni makubwa, yenye kuta pana, magumu na yenye mipaka isiyoeleweka na hutengenezwa kwenye eneo jekundu na huonekana sana kwenye mkono, kiwiliwili, ndani ya kinywa na maeneo mengine ya ngozi laini. Via:ULY CLINIC
#SOMA Zaidi kuhusu malengelenge Sehemu Za Siri;
CHANZO CHA TATIZO LA MALENGELENGE SEHEMU ZA SIRI PAMOJA NA MATIBABU YAKE