Siku ya Ukoma Duniani(World Leprosy Day (WLD).
Ikiwa ni Jumapili ya Mwisho wa Mwezi January, Shirika la Afya Duniani(WHO) pamoja na Wadau wengine wa afya wanawakumbusha watu kuhusu siku hii ya Ukoma Duniani.
Kauli mbiu ya Siku ya Ukoma Duniani 2024 ni “Beat Leprosy”. Mada hii inajumuisha malengo mawili ya siku:
- kutokomeza unyanyapaa unaohusishwa na ukoma
- na kukuza utu wa watu walioathiriwa na ugonjwa huo.
Mandhari ya kaulimbiu hii ya “Piga Ukoma(Beat Leprosy)” hutumika kama ukumbusho wenye nguvu wa haja ya kushughulikia masuala ya kijamii na kisaikolojia ya ukoma, pamoja na jitihada za matibabu za kuondokana na ugonjwa huo.
WHO: Inatoa wito kwa ulimwengu ambapo ukoma si chanzo cha unyanyapaa tena bali ni fursa ya kuonyesha huruma na heshima kwa watu wote.
Je, unaufahamu Vizuri Ugonjwa wa Ukoma?
• Soma hapa Kufahamu Ugonjwa wa Ukoma,Dalili zake pamoja na Madhara yake.